Ayatullah Khamenei aliyasema hayo Jumatano mjini Tehran wakati alipopanda miche miwili ya miti ya matunda katika bustani ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu kwa munasaba wa maadhimisho ya Wiki ya Maliasili na Siku ya Kupanda Miti nchini Iran. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, siku hii ya kupanda miti ni nembo ambayo lengo lake ni la kuhimiza utamaduni wa kupanda miti na kuzuia uharibifu wa misitu. Akifafanua zaidi kuhusu ulazmia wa kulinda mazingira na kupanda miti, Kiongozi Muadhamu alisema: "Katika kulinda misitu kunapaswa kuwepo jitihada kubwa. Taasisi husika, kama vile vyombo vya Mahakama, zinapaswa kuchukua hatua zote zinazotakiwa kuzuia kuharibiwa misitu. Ni matumaini yetu kuwa, kwa ustawi wa moyo wa kupenda miti na maeneo ya kijani kibichi, katika mustakabali nchi hii hii na watu wetu wataweza kufaidika na kadhalika Mwenyezi Mungu ataweza kuzidisha Baraka zitokanazo na mimea na mazingira ya kijani kibichi, Inshallah."