IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya Wanawake Kazakhstan

14:45 - December 26, 2019
Habari ID: 3472305
TEHRAN (IQNA) – Mashindano ya kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu yamefanyika nchini Kazakhstan katika mji wa Taraz ambapo wanawake 87 wameshiriki.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yamefanyika katika Msikiti wa Abu Bakr As-Siddiq mjini humo chini ya anuani ya 'Qur'ani, Njia Sahihi."

Qanat Jumaqul, mwakilishi wa Jumuiya za Waislamu wa Asia ya Kati na Kazakhstan ndiye aliyekuwa mkuu wa wa jopo la majaji katika mashindano hayo.

Taraz ni mji mkuu wa eneo la Jambly nchini Kazakshtan na Mto Talas unapita hapo katika eneo hilo linalopakana na Kyrguzstan.

Nchi ya Kazakhstan ni ya tisa kwa ukubwa duniani na ina eneo lenye ukubwa wa kilomita mraba 2,724,900 ambapo iko katika mabara mawili ya Asia na Ulaya. Asilimia 70 ya kwazi wa nchi hiyo ni Waislamu na lugha yake rasmi ni Kikazakh na lugha ya Kirusi pia inatumika katika idara za serikali.

3866027

captcha