IQNA

Qiraa ya Qur’ani katika misikiti Algeria kwa lengo la utulivu wakati wa janga la corona

19:19 - April 07, 2020
Habari ID: 3472642
TEHRAN (IQNA) – Wizara ya Masuala ya Kidini Algeria imetangaza kuwa, Qiraa ya Qur’ani Tukufu itasikika kupitia vipaza sauti vya misikiti yote nchini humo nusu saa kabla ya Adhana ya adhuhuri kwa lengo la kuibua hali ya kimaanawi na kudumisha utulivu wa kiroho wakati huu wa janga la COVID-19 au corona.

Uamuzi huo umechukuliwa baada ya sala zote za jamaa na Ijumaa kusitishwa kwa muda katika misikiti ya Algeria ili kuzuia kuenea ugonjwa wa corona.

Katika taarifa, Wizara ya Masuala ya Kidini ya Algeria imesema: “Uamuzi huu umechukuliwa kufuatia ombo la wananchi wa Algeria ambao wameomba kusikia Qiraa ya Qur’ani kupitia vipaza sauti vya misikiti.”

Itakumbuwa kuwa mwezi ulioipita wa Machi, Algeria ilisitisha kwa muda sala za Ijumaa na kufunga misikiti yote nchini humo kwa kama ikiwa ni katika jitihada za kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19.

Rais Abdelmajid Teboune anasema ugonjwa wa COVID-19 ni janga ambalo linatishia usalama wa taifa na amewahakikishia wananchi kuwa serikali yake itafanya kila iwezalo kukabiliana na ugonjwa huo.

Hadi kufikia 7 Aprili 2020, Algeria ilikuwa na kesi 1,423 za corona na huku waliopoteza maisha wakiwa ni 173. Algeria ilikuwa miongoni mwa nchi za kwanza barani Afrika kuripoti ugonjwa huo.

3889748

captcha