IQNA

Dereva wa Taxi India aandika Qur’ani nzima kwa mkono wakati wa zuio la corona

20:21 - October 02, 2020
Habari ID: 3473223
TEHRAN (IQNA) –Dereva wa taxi katika eneo la Hyderabad nchini India amefanikiwa kuandika nakala nzima ya Qur’ani kwa mkono katika kipindi cha miezi sita wakati wa zuio la kutotoka nje ya nyumba kufuatia kuibuka janga la corona.

Mohammad Afzal ametumia uzoefu na umahiri wake wa kuandika kwa mbinu ya kaligrafia kuandika nakala moja ya Qur’ani kwa mkono.

Anasema kutokana na shughuli yake ya kuendesha taxi hakuwa anapata muda wa kuimarisha kipaji chake cha kaligrafia lakini baada ya kuanza zuio wakati huu wa corona alipata fursa ya kuandika Qur’ani. Anasema katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani alikuwa anatumia masaa 16-18 kuandika nakala yake ya Qur’ani.

Afzal anamshukuru baba yake ambaye ndiye alimfundisha kaligrafia. Mufti wa eneo hilo Sheikh Muhiuddin Faheem amesema ni vizuri kuwa Afzal alitumia muda wa zuio kwa njia ya busara.

3472696

Kishikizo: india qurani kaligrafia
captcha