IQNA

Spika wa Bunge la Iran

Kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW ni sawa na kuwavunjia heshima Mitume wote wa Mwenyezi Mungu

14:50 - October 30, 2020
Habari ID: 3473311
TEHRAN (IQNA- Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kitendo chochote cha kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW maana yake ni kuwavunjia heshima Mitume wote na vitabu vya mbinguni.

Muhammad Baqir Qalibaf amesema hayo Alhamisi katika hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa 34 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu hapa mjini Tehran ambapo ameashiria kuhusu vitendo vya kuvunjiwa heshima Bwana Mtume SAW huko nchini Ufaransa na kusema kuwa, kitendo chochote cha kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW maana yake ni kuwavunjia heshima Mitume wote wa Mwenyezi Mungu na vitabu vya mbinguni.

Aidha amewahutubu baadhi ya watawala wa nchi za Kiislamu ambao wameanzisha uhusiano wa kawaiada na utawala haramu wa Israel na kusema kuwa, viongozi wa mataifa hayo wanapasa kutambua kwamba, hilo halitadumu lakini doa baya katika historia litabakia kwa jina lao mbele ya wananchi wa mataifa ya Kiislamu na watu huru duniani.

Qalibaf amebainisha kwamba, mambo ya pamoja ya Umma wa Kiislamu ni mengi mno kiasi kwamba, hakuna kisingizio chochote kinachobakia cha mifarakano na mivutano.

Spika wa Bunge la Iran amesema, Quds ni kibla cha kwanza cha Waislamu na moja ya mambo ya kuwaunganisha pamoja Waislamu.

Qalibaf amesema pia kuwa, Palestina itaendelea kuwa kadhia ya kwanza katika ulimwengu wa Kiislamu na kwamba, kuunga mkono malengo matukufu ya Palestina na Quds Tukufu ni jambo linaloleta mfungamano baina ya Waislamu.

Spika Qalibaf ameitaja Wiki ya Umoja kama nembo ya mshikamano wa Umma wa Kiislamu na kwamba, umoja na udugu wa Kiislamu ni moja ya misingi muhimu ya Uislamu.

3931970

captcha