IQNA

Spika wa Bunge la Iran atumia aya za Qur’an na hotuba ya Sayyid Nasrallah kufafanua kushindwa Trump

18:23 - November 08, 2020
Habari ID: 3473342
TEHRAN (IQNA) – Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amenukulu aya za Qur’ani Tukufu katika Surah An-Naziat katika kufafanua kushindwa Donald Trump katika uchaguzi wa rais Marekani mwaka huu.

Katika ujumbe aliotuma katika ukurasa wa Twitter ambapo amemfananisha Trump na firauni kwa kunukulu aya za 21-26 za Sura An-Naziat zisemazo:

 فَكَذَّبَ وَعَصَىٰ ﴿٢١﴾ ثُمَّ أَدْبَرَ يَسْعَىٰ ﴿٢٢﴾ فَحَشَرَ فَنَادَىٰ ﴿٢٣﴾ فَقَالَ أَنَا رَبُّكُمُ الْأَعْلَىٰ ﴿٢٤﴾ فَأَخَذَهُ اللَّـهُ نَكَالَ الْآخِرَةِ وَالْأُولَىٰ ﴿٢٥﴾ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبْرَةً لِّمَن يَخْشَىٰ ﴿٢٦

 “Lakini aliikadhibisha na akaasi. Kisha alirudi nyuma, akaingia kufanya juhudi. Akakusanya watu akanadi. Akasema: Mimi ndiye Mola wenu Mlezi mkuu kabisa. Basi hapo Mwenyezi Mungu akamshika kumuadhibu kwa la mwisho na la mwanzo. Kwa hakika katika haya yapo mazingatio kwa wanao ogopa.”

Qalibaf ameambatanisha aya hizo na hotuba ya Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasralah aliyetabiri kuhsindwa Trump.

Vyombo vya habari vya Marekani vimetangaza kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha cha upinzani cha Democratic, Joe Biden ndiye aliyechaguliwa na Wamarekani kuwa rais wa 46 wa nchi hiyo lakini Rais Donald Trump anasisitiza yeye ndiye mshindi na kwamba kumekuwepo wizi wa kura.

Ripoti zinasema kuwa Biden ameshinda kura 290 za wajumbe wa Electoral College baada ya kumpiku mpinzani wake, Donald Trump katika majimbo ya Pennsylvania na Nevada. Biden alihitajia kura 270 tu ya kati ya 538 za wajumbe wa Electoral College ili atangazwe mshindi. 

 

3933859

captcha