IQNA

Qalibaf: Ghuba ya Uajemi ni kipenzi cha wananchi wa Iran

16:22 - April 28, 2021
Habari ID: 3473857
TEHRAN (IQNA)- Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, kuwepo askari wa majeshi ya kigeni na wa nje ya eneo ni tishio na kunavuruga amani ya eneo.

Mohammad Baqir Qalibaf ameeleza hayo mapema leo katika hotuba aliyotoa kwenye kongamano lililofanyika kwa anuani ya "Ghuba ya Uajemi, Nyumba Yetu" na kuongeza kwamba, Ghuba ya Uajemi ni kipenzi cha wananchi wa Iran, na wananchi hao mashujaa wamewatoa wapendwa na mashujaa wao kwa ajili ya amani na usalama wa eneo hilo na dunia kwa jumla.

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ametoa salamu za pongezi kwa walinzi na askari wote wanaolinda usalama wa nchi katika eneo la Ghuba ya Uajemi na nukta hiyo muhimu ya dunia na akaongezea kwa kusema: "siku ya Ghuba ya Uajemi ni muhimu kwetu, lakini siku adhimu zaidi na ya thamani kubwa zaidi kwetu sisi, ni pale tutakaposhuhudia kuondoka vikosi vya majeshi ya kigeni katika eneo."

Qalibaf ameielezea Ghuba ya Uajemi kuwa ni moja ya maeneo hasasi, muhimu na ya kistratejia; na akasema: Leo hii uwepo wa aina yoyote wa vikosi vya majeshi ya kigeni katika eneo, si tu hakulindi na kuimarisha amani ya eneo, bali ni tishio na kuvuruga usalama wa eneo.

Spika wa Bunge la Iran ameongeza kuwa, kuwepo majeshi ya kigeni yakiongozwa na ya Marekani kumevuruga usalama na kusababisha kupotea fursa za kiuchumi katika eneo na nje ya eneo la Ghuba ya Uajemi.

Qalibaf amebainisha pia kwamba, siku majeshi yote ya kigeni yatakapoondoka katika eneo la Ghuba ya Uajemi, bila shaka itakuwa siku ya furaha kwa watu wa eneo hili na akaongeza kuwa, taifa la Iran limetoa mhanga mashahidi wengi katika eneo kwa ajili ya kudhmaini usalama wa eneo lenyewe la Ghuba ya Uajemi na usalama wa dunia.

/3967728

Kishikizo: Qalibaf iran ghuba
captcha