IQNA

Maonyesho ya Qur’ani yanafanyika Sharjah

21:11 - December 22, 2021
Habari ID: 3474708
TEHRAN (IQNA)- Maonyesho ya Misahafu ya kale yanafanyika katika mjini Sharjah Umnoja wa FALME ZA Kiarabu (UAE) katika Chuo kikuu cha Sharjah, Tawi la Kalba.

Maonyesho hayo yaliyopewa jina la “Maonyesho ya Kitaifa ya Misahafu na Miradi  ya Wajasirimali Wadogo” yanafanyika kwa ushirikiano na Baraza la Wazazi katika sherehe iliyodhuhuriwa na Sheikh Haitham bin Saqr al Qasimi, naibu mkuu wa ofisi ya mtawala wa Sharjah eneo la Kalba.

Dkt. Ali Obaid, Naibu Mkuu  wa Chuo Kikuu cha Sharjah amesema idadi kubwa ya idara za serikali  na sekta binafsi zimeshiriki katika maonyesho hayo. Imedokezwa kuwa maonyesho haya yana vibanda 45 vya miradi mbali mbali ya sanaa za mikono na Misahafu.

3477045/

captcha