IQNA

Msikiti wa Jamia Algeria ni wa tatu kwa ukubwa dunaini

TEHRAN (IQNA)- Msikiti wa Jamia Algeria, ambao pia ni maarufu kama Masjid Djamaa el Djazaïr ni msikiti wa tatu kwa ukubwa duniani. Mnara wake wenye urefu wa mita 267 ni moja kati ya minara mirefu zaidi duniani.

Msikiti huo ulio katika mji mkuu Algiers, una uwezo wa kubeba waumini  120,000.