IQNA

Al-Azhar yapongeza sera za Canada za chuki dhidi ya Uislamu

18:23 - February 01, 2022
Habari ID: 3474879
TEHRAN (IQNA) – Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar nchini Misri kimepongeza uamuzi wa serikali ya Canada kutangaza siku maalumu ya kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu.

Ofisi ya Kufuatilia Chuki Dhidi ya Uislamu (Islamophobia) katika Chuo cha Kiislamu cha Al Azhar imesema hatua za kukabiliana na ubaguzi na chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu zinapaswa kupongezwa.

Taarifa hiyo imesema Islamophobia ni aina ya ubaguzi na ni chanzo cha kuenea misimamo mikali na ugaidi.

Al Azhar aidha imetoa wito kwa nchi zingine za Magharibi zifuate hatua sawa na zilizochukuliwa na Canada kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu.

Katika hotuba kwa mnasaba wa mauaji kwa ufyatuaji risasi katika msikiti mjini Quebec, Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau amelaani vitendo dhidi ya Uislamu nchini humo na kusema kuwa serikali yake imaamua kutangaza Januari 29 kuwa ni siku ya kitaifa ya kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu.

Ikumbukwe kuwa Waislamu sita – Aboubaker Thabti, Abdelkrim Hassane, Khaled Belkacemi, Mamadou Tanou Barry, Ibrahima Barry na Azzedine Soufiane – waliuawa wakati gaidi Bissonnette alipofyatua risasi ndani ya Kituo cha Kiislamu cha Quebec Januari 29 2017.

Hujuma hiyo ilijiri baada ya Swala ya Ishaa ambapo waumini wengi walijeruhiwa.

4032805

captcha