IQNA

Waziri wa Algeria asisitiza nafasi ya misikiti katika kuzuia misimamo mikali

16:56 - February 22, 2022
Habari ID: 3474962
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kidini Algeria amesisitiza kuhusu nafasi muhimu ya misikiti katika kuzuia misimamo mikali ya kidini na utumiaji mabavu.

Akizungumza alipotembelea msikiti wa Bordj Bou Arreridj kaskazini mwa nchi, Youssef Belmehdi amesisitiza kuhusu nafasi ya misikiti na vyuo vya Qur'ani katika kuimarisha utambulisho wa kitaifa Algeria.

Aidha amesema wizara yake imejenga misikiti na vituo vya Kiislamu kwa msaada wa wafadhili na kuongeza kuwa, serikali ya sasa ya Algeria ina azma ya kuutumikia Uislamu.

Belmehdi amesema kuanzisha shule za Qur'ani na kufunguliwa misikiti ni moja ya njia za kueneza fikra za misimamo ya wastani na amani na kuzuia misimamo mikali ya kidini.

Halikadhalika amesema wizara yake iko tayari kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kuongeza kuwa shughuli zote za ibada misikiti zitafanyika kwa kuzingatia kanuni za kiafya zilizowekwa ili kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19.

4038077

Kishikizo: algeria qurani tukufu
captcha