IQNA

Waislamu Ulaya

Jumuiya ya Waislamu Ireland waalika umma 'Kutuuliza Chochote'

22:48 - August 20, 2022
Habari ID: 3475653
TEHRAN (IQNA) – Jumuiya ya Waislamu huko Cork, jiji la pili kwa ukubwa nchini Ireland, imewaalika watu kuwauliza maswali yoyote wangependa kuhusu Uislamu au mtindo wa maisha wa Waislamu katika hafla maalum ya Kiislamu ya 'mlango wazi'.

Ali Hamou, mmoja wa waandaaji wa hafla hiyo, alisema wamefungua milango Uislamu na maisha ya Waislamu katika maonyesho ya utamaduni wa Kiislamu katika Hoteli ya Imperial ya mji huo kwa matumaini ya kufuta dhana potofu kuhusu Uislamu na Waislamu

Hafal hiyo imefanyika kwa ushurikiano wa kikundi cha Discover Islam, na imejumuisha maonyesho ya nakala mbalimbali za Qur’ani Tukufu katika tafsiri za moja kwa moja, Kitabu cha Uislamu, na Kijitabu cha Seerah.

Pia kulikuwa na maoneysho mbalimbali ya kitamaduni, picha za kuchora, maandishi ya Kiislamu, kaligrafia ya Kiarabu, na mavazi ya kitamaduni ya Kiislamu.

Hamou alisema: "Tumeonyesha utamaduni wetu, dini yetu, sanaa yetu, vyakula na mavazi, na tumewaalika watu kutuuliza chochote unachoweza kufikiria.

"Watu wana mamia ya maswali, na tunapata maswali muhimu sana, lakini bado, tunapata maswali ya kutatanisha kama 'unamjua Bin Laden?' au 'unawajua ISIS (Daesh)?'.

“Watu wanaposikia mashambulizi ya kigaidi, ghafla kila Muislamu ni gaidi lakini ukweli ni kwamba pengine umewahi kutibiwa nyumbani hapa na daktari au nesi Muislamu ambaye aliokoa maisha."

"Ukirejea katika historia, Waairishi pia wamekuwa wahasiriwa wa dhana potofu.

"Tukio hili ni fursa nzuri kwetu kufuta dhana hizo potofu, na watu kutufahamu."

Inakadiriwa kuwa kuna Waislamu wapatao 5,000 wanaoishi na kufanya kazi katika eneo kubwa la Cork.

3480162

captcha