IQNA

Mfumo wa kifedha wa Kiislamu

Ukuaji wa haraka watabiriwa kwa mfumo wa kifedha Kiislamu

12:37 - August 28, 2022
Habari ID: 3475693
TEHRAN (IQNA) - Utafiti mpya umegundua kuwa mfumo wa kifedha wa Kiislamu unastawi kwa kasi na uko tayari kwa ukuaji wa haraka katika miaka ijayo.

Ripoti ya Global Islamic Fintech ya 2022 iligundua kuwa soko la kimataifa la mfumo wa kifedha wa Kiislamu lilikuwa kwa thamani ya U$79bn mwaka wa 2021,   na likichukua asilimia 0.8 ya jumla ya soko la kimataifa la kifedha,

Ripoti hiyo - ambayo imetayarishwa na Dinar Standard na Ellipses - ilitabiri kuwa ukubwa wa soko la Kiislamu la fintech unatarajiwa kufikia US$179bn ifikapo 2026.

"Pamoja na msukosuko wa kijamii na kiuchumi na mabadiliko ya kijiografia ya kisiasa yaliyoletwa na janga la kimataifa la COVID-19 na vita vinavyoendelea nchini Ukraine, mfumo wa kifedha wa  Kiislamu kwa sasa unaweza kuwa na nafasi kubwa katika mfumo jumla wa kifedha na pia kichocheo chenye ushawishi cha ushirikishwaji wa kifedha duniani," alisema mwakilishi wa Qardus Ali Ismail.

"Ikiwa mfumo wa kifedha wa Kiislamu utaendelea katika njia ile ile ya ukuaji wa haraka ambayo imekuwa imekuwa ikishuhudiwa kwa muda mrefu, sekta hiyo bila shaka itaibuka mshindani mkubwa hasa Magharibi, Asia na hivi karibuni zaidi barani Afrika katika robo karne iliyopita.

Ripoti ya Global Islamic Fintech ya mwaka 2022 pia iligundua kuwa asilimia 75 ya vijana wa Kiislamu wanataka benki zao kufanya uwekezaji ambao 'unafanya mema duniani', huku asilimia 62 wakipinga benki zao kukopesha makampuni ya tumbaku na asilimia 69 hawataki benki zao zikopeshe taasisi za kamari. .

Asilimia 74 ya vijana wa Kiislamu walisema ni muhimu kupata huduma za benki zao kupitia programu ya simu.

Mfumo wa kifedha wa Kiislamu unashughulikia uwekezaji unaoenda kwa mujibu wa sheria za Kiislamu na haujihusishi na  malipo ya riba na kuwekeza katika biashara zinazohusiana na pombe, tumbaku na kamari miongoni mwa zingine zilizo kinyume cha mafundisho wa Kiislamu.

captcha