IQNA

Waislamu wa Madhehebu ya Shia

Kikao cha Jumuiya ya Kimataifa ya Ahl-ul-Bayt (AS) chajadili changamoto za uenezaji Uislamu

20:06 - September 04, 2022
Habari ID: 3475731
TEHRAN (IQNA) – Mkutano wa Saba wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Kimataifa ya Ahl-ul-Bayt AS ulimalizika hapa katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran siku ya Jumamosi.

Kikao cha Jumuiya ya Kimataifa ya Ahl-ul-Bayt (AS) chajadili changamoto za uenezaji Uislamu

TEHRAN (IQNA) – Mkutano wa Saba  wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Kimataifa ya Ahl-ul-Bayt AS ulimalizika hapa katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran siku ya Jumamosi.

Mkusanyiko huo ulifanyika Tehran na katika mji mtakatifu wa kaskazini mashariki mwa Iran wa Mashhad kwa kauli mbiu ya “Ahl-ul-Bayt (AS); Mhimili wa Uadilifu, Haki na Heshima ya Mwanadamu”.

Mamia ya wageni kutoka nchi zaidi ya 110 walishiriki katika kusanyiko hilo.

Katika siku ya mwisho ya tukio, wazungumzaji walijadili changamoto na matatizo ambayo Waislamu wa madhehebu ya Shia wanakabiliana nayo katika njia ya kueneza mafundisho ya Ahl-ul-Bayt (AS).

Inafaa kuashiria hapa kuwa, Ahl-ul-Bayt (AS) inamaanisha watu wa nyumba ya Mtume Muhammad (SAW)

Kati ya waliohutubu katika kikao hicho ni  Muhammad Haidar kutoka Mali, ambaye alisema Tabligh (uenezi) katika kila jamii ina mahitaji yake.

Alibainisha kuwa kufaidika na nafasi ya mtandao kwa Tabligh kunaweza kuwa na ufanisi mkubwa kutokana na jinsi vijana wanavyotumia mtandao.

Zayd al-salami kutoka Australia alifafanua kuhusu shughuli za Waislamu wa Madhehebu ya Shia nchini mwake pamoja na suala la chuki dhidi ya Waislamu wa madhebu ya Shia na pia chuki jumla dhidi ya Waislamu wote katika nchi hiyo..

Katika hotuba yake, Mustafa Ghulam Abbas kutoka Kuwait alipendekeza kuundwa kwa mkutano wa wanazuoni ili kutatua tofauti kati ya Mashia.

Baadaye katika siku ya mwisho ya mkusanyiko, maamuzi yaliyofanywa katika tume tofauti yalitangazwa.

Kati ya maamuzi hayo ni kutumia uwezo wa kisheria uliopo katika nchi tofauti kurejesha haki za madhehebu ya Shia, kukuza uhusiano kati ya Mashia kiutamaduni, kiuchumi, kijamii na kisiasa, kuanzisha vuguvugu la kukuza ufahamu wa Uislamu katika vyombo vya habari, kufundisha vijana kuhusu kutumia mitandao ya kijamii kwa njia sahihi, kufanya mikutano kati ya wanaharakati wa kiuchumi, na kuunda mtandao wa wanawake wa Kishia ambao wanashiriki katika nyanja za kiuchumi.

Miongoni mwa maamuzi mengine yaliyofanywa katika mkutano huo ni uanzishwaji wa vituo vya utafiti na maendeleo.

Jumuiya ya Kimataifa ya Ahl-ul-Bayt (AS) ilianzishwa mwaka 1990 na kundi la wasomi wa Shia ili kutambua, kupanga, kuelimisha na kusaidia wafuasi wa Nyumba ya Mtume Muhammad (SAW).

4082943

captcha