IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Suala la maendeleo ya kisayansi na kuvuka mipaka ya elimu halipasi kusahaulika

16:59 - January 02, 2023
Habari ID: 3476348
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza katika mazungumzo na wawakilishi wa Baraza Kuu la Muungano wa Jumuiya za Wanachuo wa Kiislamu barani Ulaya kuwa suala la maendeleo ya kisayansi na kuvuka mipaka ya elimu halipasi kusahaulika.

Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema leo Jumanne alipoonana na wawakilishi wa Baraza Kuu la Muungano wa Jumuiya za Wanachuo wa Kiislamu barani Ulaya kuwa, jumuiya za Kiislamu ni moja ya utajiri wa Jamhuri ya Kiislamu na zenye majukumu ya kipekee na kusisitiza kuwa, majukumu muhimu ya jumuiya za Kiislamu ni kuendeleza njia thabiti, kuacha athari katika mazingira yanayozizunguka na kubainisha ujumbe mpya wa Jamhuri ya Kiislamu.

Kitengo cha habari cha Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kimeripoti kuwa, Ayatullah Khamenei amemuenzi kwa kumkumbuka marhum Hujjatul Islam wal Muslimin Dakta Eje'i mmoja wa waasisi wa Muungano wa Jumuiya za Kiislamu za Wanachuo barani Ulaya na akapongeza harakati za vijana wanachuo kuwa zenye mitazamo mipya na ya kimapinduzi. 

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, Jumuiya za Kiislamu zimeundwa kwa lengo la kuimarisha misingi yake ya kifikra na kiitikadi na pia kuathiri mazingira yanayozizunguka, hata hivyo jumuiya za kiislamu nje ya nchi zina kazi na majukumu mengine pia ambayo ni kuarifisha fikra za msingi na kuu za Jamhuri ya Kiislamu.   

Katika mazungumzo hayo, Ayatullah Khamenei amelitaja suala la elimu na maendeleo ya kisayansi kuwa ni jambo ambalo limekuwa likizungumziwa kwa pamoja hapa nchini katika miaka ya hivi karibuni, na akapongeza kufanyika  mkutano wa kisayansi katika Kongamano la hivi sasa la Jumuiya za Wanachuo wa Kiislamu barani Ulaya. Ameongeza kuwa, suala la maendeleo ya kisayansi na kuvuka mipaka ya kielimu halipasi kusahaulika na kudhaniwa kuwa, kutiliwa maanani nyuga za kidini na kimapinduzi kunasababisha kughafilika katika masuala ya maendeleo ya kisayansi. 

4111568

captcha