Imeandaliwa na Kituo cha Wanaharakati wa Vyombo vya Habari vya Ulimwengu wa Kiislamu kwa usaidizi wa Jukwaa la Kimataifa la Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu.
Wanaharakati wakuu wa vyombo vya habari na wasomi wa kidini kutoka zaidi ya nchi 20 wamehudhuria hafla hiyo wakijadili masuala yanayohusiana na umoja wa Umma wa Kiislamu, ujuzi wa vyombo vya habari, na uwezo wa vyombo vya habari vya kimataifa.
Ni moja katika mfululizo wa mikusanyiko ya kimataifa inayoitwa Kongamano la Kimataifa la Mnara.
Washiriki wa hafla ya leo katika taarifa yao wamelaani vitendo vya hivi karibuni vya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu na matukufu ya Kiislamu katika nchi za Ulaya.
Walitaja hatua hizo za kufuru kuwa matendo ya aibu ambayo hakuna sheria au mantiki inayounga mkono.
Hatua hizo zinaumiza hisia za mabilioni ya Waislamu na watu mashuhuri duniani na kuibua chuki na mifarakano, walisema.
Taarifa hiyo pia ilizikashifu serikali za Magharibi kwa kupandikiza mbegu za chuki na uhasama na kuchochea moto wa ghasia duniani.
Ilisisitiza kwamba Waislamu, kwa msingi wa imani yao ya kidini, kamwe hawajiruhusu kutukana utakatifu wa imani nyingine na kwamba wafuasi wa Uislamu wanaviheshimu sana vitabu na manabii wote wa Mungu.
4118238