IQNA

Mapinduzi ya Kiislamu

Kiongozi Muadhamu ametoa msamaha na punguzo la vifungo kwa makumi ya maelfu ya watuhumiwa na wafungwa

7:42 - February 06, 2023
Habari ID: 3476518
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa msamaha na punguzo la vifungo kwa makumi ya maelfu ya watuhumiwa na wafungwa kwa mnasaba wa kuwadia maadhimisho ya miaka 44 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na sikukuu za mwezi wa Rajab.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameidhinisha pendekezo la Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran, Gholam Hossein Mohseni Ejei la kupunguziwa vifungo au kuachiwa huru makumi ya maelfu ya wafungwa wa Kiirani waliokuwa wakitumikia vifungo katika magereza mbalimbali hapa nchini.

Miongoni mwa walionufaika na msamaha huo wamo watu waliokamatwa katika miezi ya hivi karibuni kwa kosa la kushiriki katika fujo na vurugu zilizoibuka kwa kisingizio cha kifo cha binti wa Kikurdi Mahsa Amini.

Katika barua yake kwa Kiongozi Muadhamu, Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran, Gholam Hossein Mohseni Ejei amesema: Katika matukio ya hivi karibuni baadhi ya wananchi hususan vijana walifanya vitendo visivyo sahihi kutokana na kuathirika na propaganda za maadui na hivi sasa wengi wao wamejuta kwa vitendo hivyo na wanaomba msamaha hasa baada ya kufahamika njama za maadui wa kigeni na makundi yaliyo dhidi ya Mpainduzi ya Kiislamu.

Sura ya 110 ya Katiba ya Iran inampa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu haki ya kupunguza au kuwasamehe wafungwa kutokana na pendekezo la Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

4119858

captcha