IQNA

Mashindano ya Qur'ani Tukufu

Misri yawataja washindi wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu

20:48 - February 08, 2023
Habari ID: 3476533
TEHRAN (IQNA) - Washindi wa Mashindano ya 29 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu nchini Misri walitangazwa na jopo la waamuzi.

Jumla ya wahifadhi na wasomaji Qur'ani Tukufu 108 kutoka nchi 58 zikiwemo nchi 33 za Afrika wamehudhuria hafla hiyo ya kimataifa.

Mashindano hayo yaliyopewa jina la marehemu Qari Sheikh Mustafa Ismail, yalianza katika mji mkuu wa Misri Jumamosi, Februari 4.

Wataalamu saba wa Qur'ani Tukufu kutoka Misri, Jordan, Palestina, Saudi Arabia, Sudan, Chad na Oman walikuwa wajumbe wa jopo la waamuzi.

Washindi katika makundi mbalimbali ni kama wafuatao:

Maher Mohammad Abdul Nabi Farmawi kutoka Misri na Abdullah Izzedin Abdul Rahman walikuja wa kwanza na wa pili katika kategoria ya kwanza, ambayo ni kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu na kuelewa maana ya aya zake kwa wanaume na wanawake walio chini ya miaka 45. Mshindi na mshindi wa pili atapata Pauni 250,000 na 150,000 za Misri mtawalia.

Kundi la pili ni kuhifadhi Qur'ani Tukufu na kuelewa aya zake kwa familia. Angalau watu watatu wa kila familia wanapaswa kuwa wahifadhi Qur'ani Tukufu. Ahmed al-Ziyat, Saleh al-Ziyat na Khanum al-Ziyat ni washiriki wa familia iliyoshinda ambao watatunukiwa Pauni 250,000 za Misri.

Kundi la tatu ni kuhifadhi, kufasiri na matumizi ya aya za Qur'ani Tukufu  katika sayansi nyinginezo kwa washiriki walio chini ya umri wa miaka 45. Mshindi alikuwa Mohamd Ahmed Abdul Ghani Daghidi kutoka Misri ambaye atapokea Pauni 150,000 za Misri.

Kuhifadhi Qur'ani Tukufu kwa mbinu saba za qiraa kwa washiriki walio chini ya umri wa miaka 50 ni kategoria inayofuata yenye zawadi ya juu ya Pauni 150,000 za Misri. Mshindi katika kitengo hiki ni Hamada Mohamed al-Sayyed Khatab kutoka Misri.

Abdul Samad Adam kutoka Ghana na Fatima Shaya Zahir kutoka Maldives walikuja wa kwanza na wa pili katika kategoria ya tano, ambayo ni kuhifadhi Qur'ani Tukufu kwa wasiozungumza Kiarabu walio chini ya umri wa miaka 40. Wametunukiwa Pauni 150,000 na 100,000 za Misri, mtawalia.

Kundi linalofuata ni kuhifadhi Qur'ani Tukufu kwa watu wenye ulemavu. Washiriki walipaswa kuwa chini ya miaka 35. Asma Adil Sayyed Ahmed alikuja wa kwanza na atatwaa Pauni 100,000 za Misri.

Katika kundi la saba, kuhifadhi Qur'ani Tukufu na kuelewa msamiati na tafsiri yake kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 15, Mana Ahmed Saad Abbas Muhaysan kutoka Misri alitajwa kuwa mshindi na atapata Pauni 100,000 za Misri.

Kategoria ya mwisho ni maalum kwa aliyekuwa bora zaidi katika kuhifadhi Qur'ani Tukufu na mshindi alikuwa Mustafa Muhammad Mustafa Abdullah kutoka Misri.

 

3482402

captcha