IQNA

Mwezi wa Ramadhani

Kuwait yaanza maandalizi ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

19:00 - February 14, 2023
Habari ID: 3476561
TEHRAN (IQNA)- Huku mwezi mtukufu wa Ramadhani ukitazamiwa kuanza Machi 23, Wizara ya Wakfu ya Kuwait imeanza maandalizi yake ya awali ya kuupokea mwezi huu mtukufu, na kuandaa misikiti kwa ajili ya kupokea maelfu ya waumini kuswali sala ya Taraweh na sala nyingine za jamaa katika mwezi huu.

Duru za habari zinadokeza kuwa Wizara ya Wakfu ya Kuwait imezidisha juhudi zake za kujenga mazingira ya imani na kuhakikisha waumini wana utulivu na usalama katika misikiti zaidi ya 1,590 nchini humo. Waziri wa Wakfu Abdulaziz Al-Majed amesisitiza wakati wa mkutano wake na maafisa wa wizara yake wiki iliyopita kuhusu hitajio la juhudi za pamoja, na kuwataka wakurugenzi wa misikiti katika majimbo sita kufanya usalama wa waumini na utulivu kuwa vipaumbele vyao kuu.

Vyanzo hivyo vilieleza kuwa taratibu maarufu zaidi zitakazotumika kulinda misikiti wakati wa Ramadhani ni kuzuia ombaomba, kudhibiti ukusanyaji wa michango kwa taratibu zilizoidhinishwa na Wizara ya Masuala ya Kijamii, kulinda magari ya waumini dhidi ya wizi, na kudhibiti msongamano wa magari mbele ya misikiti.

Aidha imedokezwa kuwa, Wizara ya Wakfu itaomba msaada wa wasomaji Qur'ani Tukufu kutoka nje ya nchi mwaka huu, pamoja na kuruhusu kuandaliwa futari misikiti kwa sharti kuwa futari iandaliwe katika uwanja wa msikiti na si ndani.

3482469

captcha