IQNA

Harakati za Qur'ani

Maonesho ya 16 ya Kimataifa Qur'ani Tukufu yapangwa Katika Haram Tukufu ya Imam Ridha huko Mashhad

20:16 - February 25, 2023
Habari ID: 3476621
TEHRAN (IQNA) – Toleo la 16 la Maonesho ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Mashhad yatafanyika katika Haram ya Imam Ridha (AS) katika mji wa kaskazini mashariki mwa Iran, afisa mmoja alisema.

Hamid Samadi, Naibu wa Idara ya Qur'ani na Etrat ya Idara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu katika Mkoa wa Khorasan Razavi, aliiambia IQNA kwamba tarehe kamili ya maonyesho bado haijabainishwa.

Mlango wa kuingia kwa Bab al-Jawad (AS) utakuwa mwenyeji wa maonyesho hayo, ambayo yatafanywa na idara hiyo, alisema.

Hafla hiyo ya kimataifa ya Qur'ani huandaliwa kila mwaka katika mwezi mtukufu wa Ramadhani unaotarajiwa kuanza Machi 23 mwaka huu.

Samadi alisema pia kuna maonyesho mengine yanayotarajiwa kufanyika Mashhad mwezi ujao wakati idadi kubwa ya wafanyaziara wanatarajiwa kuzuru mji huo mtakatifu wakati wa likizo ya Nowruz yaani mwaka mpya wa Kiirani.

Alisema kuwa maonyesho yenye jina la "Katika Njia ya Peponi", yataandaliwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Kiislamu kwa ushirikiano na mashirika mengine ya majimbo.

Maonyesho sawia ya Qur'ani huandaliwa wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika miji mingine ya Iran kila mwaka ikiwa ni pamoja na Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran, ambayo yanalenga kukuza dhana za Qur'ani na kuendeleza shughuli za Qur'ani Iran na dunia nzima.

4123780

captcha