IQNA

Mwezi wa Ramadhani

Nakala Milioni Moja za Qur'ani Tukufu kusambazwa katika nchi 22 Mwezi wa Ramadhani

17:50 - March 07, 2023
Habari ID: 3476673
TEHRAN (IQNA) - Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Saudia imesema inapanga kusambaza nakala milioni moja za Qur'ani Tukufu katika lugha tofauti katika nchi 22.

Misahafu hiyo itasambazwa wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na inajumuisha tarjuma ya Qur'ani Tukufu katika lugha 76, ripoti hiyo ilisema, na kuongeza kuwa zitasambazwa kati ya vituo vya kidini na Kiislamu pamoja na ofisi zinazohusika na wizara hiyo.

Nakala hizo za Qur'ani Tukufu  zimechapishwa katika KIituo cha Mfalme Fahd kwa ajili ya Uchapishaji wa Qur'ani Tukufu, ambalo liko katika mji mtakatifu wa Madina.

Kituo hicho huzalisha  takriban nakala milioni 10 za Qur'ani Tukufu  kila mwaka. Pia huchapisha tafsiri na tarjuma ya Qur'ani Tukufu katika lugha mbalimbali.

Ramadhani (itakayoanza Machi 23 mwaka huu) ni mwezi wa tisa katika kalenda ya Kiislamu. Ni kipindi cha Sala, Saumu, utoaji wa sadaka kwa Waislamu duniani kote.

Wakati wa Ramadhani, Waislamu hufunga (kujiepusha na vyakula na vinywaji) kuanzia Alfajiri  hadi Magharibi. Pia wanatumia muda mwingi katika mwezi huu kusoma na kutafakari kuhusu Qur'ani Tukufu.

4126295

Kishikizo: misahafu qurani tukufu
captcha