IQNA

Spika wa Bunge la Iran

Maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka hii yalikuwa na taathira kubwa

20:57 - April 16, 2023
Habari ID: 3476876
TEHRAN (IQNA)- Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema: "kuhudhuria kwa hamasa kubwa wananchi wa Iran katika maandamano ya Siku ya Quds Duniani bila shaka kumeyafanya maandamano ya mwaka huu kuwa moja ya maandamano yenye msisimko na taathira kubwa zaidi katika miaka ya hivi karibuni na kuwapa faraja Mujahidina wanaopambana katika njia ya ukombozi wa Quds."
Mohammad Baqer Qalibaf, Spika wa Bunge la Iran ameyasema hayo mapema leo katika kikao cha wazi cha Bunge na kuongeza kuwa: Ubunifu aliofanya Imam Khomeini, mwasisi mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, -ambao ni kigezo halisi cha muqawama dhidi ya dhulma na ubeberu wa utawala wa Kizayuni-, wa kuitangaza Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu Ramadhani kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds, kila mwaka huwapa moyo na kuwafariji Mujahidina wanaopambana kwa ajili ya ukombozi wa Quds Tukufu.
Spika wa Majilisi ya Ushauri ya Kiislamu ameongeza kuwa: Mwaka huu wananchi wa Iran waling'ara kwa namna maalumu na ya kihistoria na kuutikisa mhimili wa adui Mzayuni kote nchini kuanzia kwenye miji mikubwa hadi vijiji vidogovidogo.

Takriban miaka 44 iliyopita tarehe 13 Ramadhani 1399 Hijria Qamaria sawa na tarehe 16 Mordad 1358 Hijria Shamsia, Imam Khomeini (MA), Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, kwa mtazamo wa hekima na busara uliotambua ulazima wa kuwepo harakati ya wananchi duniani kwa ajili ya ukombozi wa Palestina na kutokomezwa dondandugu la saratani ya Israel aliitangaza Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds.

Ijumaa iliyopita, katika Siku ya Quds Duniani, wananchi wa Iran na wa baadhi ya nchi duniani walitangaza uungaji mkono wao kwa wananchi madhulumu wa Palestina na kuchukizwa kwao na utawala ghasibu wa Kizayuni kwa kuhudhuria kwa wingi katika maandamano na mikusanyiko ya siku hiyo.
4134436
Kishikizo: Qalibaf siku ya quds
captcha