Mamlaka zimekuwa zikisimamia wimbi la waumini waliofika kwenye misikiti hiyo miwili mitakatifu wakati wa mwezi wa Ramadhani, mojawapo ya nyakati zenye shughuli nyingi zaidi za mwaka.
Zaidi ya wageni milioni moja walikuwepo kwenye Msikiti Mkuu wa Makka siku ya Jumapili.
Urais Mkuu wa Masuala ya Msikiti Mkuu na Msikiti wa Mtume (saww) alisema kulikuwa na wafanyakazi 4,000 kwenye Msikiti Mkuu na kwamba msikiti huo ulikuwa ukisafishwa usiku na mchana na timu 70 za wahudumu.
Mpango mpya ulizinduliwa katika Msikiti Mkuu ili kuboresha huduma kwa wageni wakiwemo wazee na walemavu.
Mradi huo ni sehemu ya kampeni ya “Ni Heshima Kuwahudumia Mahujaji Wetu” ambayo inaonekana kuhakikisha waumini wanapata huduma bora zaidi kuanzia wanapowasili hadi wanapoondoka. Aghalabu ya waumini wanaofika Makka wakati huu hutekelelza ibada ya Hija ndogo ya Umrah
Mkuu wa ofisi ya rais, Abdulrahman Al-Sudais, aliongoza waumini katika sala za usiku mjini Makka.
3483253