IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Washindi wa Mashindano ya Qur'ani huko Sharjah, UAE, watunukiwa

15:11 - May 01, 2023
Habari ID: 3476943
TEHRAN (IQNA) – Mashindano ya Qur’ani yaliyoandaliwa na Baraza la Kitongoji la Al Suyoh la Idara ya Masuala ya Wilaya na Vijiji ya Sharjah nchini Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) yamehitimishwa.

Mashindano hayo yaliwalenga watoto wa wakaazi wa kitongoji hicho, yakilenga kuwahimiza watoto kusoma Qur'ani Tukufu.

Mashindano hayo yaliyofanyika katika toleo lake la kwanza, yamefanikiwa kuwapa motisha washiriki 24 wenye umri wa kati ya miaka mitano hadi kumi na nne kwa kuchukua video hizo huku wakisoma aya za Qur'ani Tukufu.

Ikiwa ni sehemu ya azma ya Baraza hilo kuhimiza watoto kutoka vitongojini kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu, Baraza la Kitongoji cha Al Suyoh lilifanya hafla katika Makao Makuu ya Baraza hilo mjini Sharjah, kuwaenzi washindi na washiriki, mbele ya Youssef Obaid Harmoul Al Shamsi , Mwenyekiti wa Baraza la Kitongoji cha Al Suyoh, waheshimiwa kadhaa, pamoja na idadi kubwa ya waalikwa na familia.

Sherehe hiyo ilishuhudia kuenziwa washindi wa nafasi za kwanza, wakiwemo washiriki wote katika kategoria za shindano, pamoja na jury.

Akizungumzia hili, Mwenyekiti wa Baraza la Kitongoji cha Al Suyoh alisisitiza nia ya Baraza hilo kupitisha matukio kama hayo ambayo yanakuza mshikamano wa kijamii kati ya watu wa kitongoji hicho, akipongeza mafanikio ya ajabu ya shindano hilo ambalo linatafsiri dira ya baraza hilo.

3483387

Kishikizo: qurani tukufu uae
captcha