Akigusia safari ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Syria, Ayatullah Seyed Ahmad Khatami, Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran ameongeza kuwa: Ziara hii ni uthibitisho mwingine wa misimamo imara ya mrengo wa muqawama au mapambano; hasa kwa vile Syria iko mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni."
Ayatullah Khatami amesema: "Hatua ya wananchi wa Syria kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa namna ya kipekee kwa hakika ni kulienzi na kulitukuza taifa la Iran na kunaonyesha mafungamano makubwa kati ya mataifa haya mawili na shukrani za Wasyria kwa uungaji mkono wa taifa la Iran wakati nchi hiyo ilipokuwa ikikabiliana na dhulma."
Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema: "Kuzidi kuimarika uhusiano kati ya Iran na Syria katika nyanja zote kumedhihirisha kuzaa matunda nasaha za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu za kuendelea kuupinga utawala ghasibu wa Kizayuni, kwani madola yote yalikuwa dhidi ya Syria na nchi pekee iliyosimama karibu na Syria, ilikuwa ni Iran ya Kiislamu."
4138649