IQNA

Turathi

Msikiti wenye Mnara Uliopinda ni kivutio cha Utalii Nchini Qatar

15:38 - May 31, 2023
Habari ID: 3477075
TEHRAN (IQNA) – Msikiti nchini Qatar wenye mnara wa kipekee unaoegemea unazidi kuzingatiwa mtandaoni na kuwa kivutio cha watalii.

Uko katika jiji Al Shahaniya, umepewa jina la utani la 'Msikiti Uliopinda wa Doha'.

Muundo huo unalinganishwa na Mnara maarufu wa Pisa, nembo ya kitalii ya Kiitaliano inayojulikana kupinda chini ya daraja nne.

Sheikh Faisal bin Qassim Al Thani, mtendaji mkuu wa mojawapo ya makampuni makubwa ya Qatar Al Faisal Holding, ndiye aliyekua na ubaunfu wa usanifu majengo katika msikiti huo.

Alisema alifikiria kuhusu kujenga msikiti ambao utakuwa tofauti na misikiti mingine duniani, pamoja na mnara wake unaochanganya mila na usasa na kuashiria uwepo wa kipekee katika mandhari.

"Tulijenga mnara uliopinda na tumezingatia usanifu majengo wa jadi wa Kiislamu, kutambua historia tajiri ya usanifu wa Qatar, na kuwasilisha sura ya kipekee ya jengo letu," alisema Sheikh Faisal.

"Kito hiki cha usanifu sio tu kinavutia watalii na wageni kwa taifa letu, lakini pia kinaashiria hamu yetu ya kujumuisha mambo ya kitamaduni na muundo wa kisasa."

 Ujenzi wa muundo huo wa kipekee ulichukua zaidi ya mwaka mmoja na awamu ya mwisho kukamilika mnamo 2022.

Msikiti Uliopinda umesimama kando ya Makumbusho ya Sheikh Faisal bin Qassim Al Thani na Hoteli ya Al Samriya.

Bi Gritsenko, ambaye alihamia Qatar kutoka Armenia mwaka mmoja uliopita, alichapisha video ya msikiti huo uliopinda kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii ambapo idadi kubwa ya marafiki na familia waliuliza maswali kuhusu muundo huo.

“Wengine waliniuliza ikiwa ni hitilafu ya ujenzi au tetemeko la ardhi liliufanya mnara kupinda.

"Lakini nilifafanua kuwa ilikuwa muundo tu, kama mnara wa Pisa," alisema Bi Gritsenko.

Nivedita Vishwanathan, mtaalamu wa fiziotherapi aliyeishi Doha alishangaa kuona video ya msikiti huo.

"Niliona usanifu huo unashangaza kabisa.

Mnara huo una mashine ndogo  30 zenye uwezo wa kubaini matatizo hisia ya juu ambazo huhifadhi usalama wa muundo kwa kufuatilia uzito na mwelekeo.

Juu ya mnara huo kuna hilali iliyotengenezwa kwa shaba ya kale ya Misri.

Jiwe lililotumika katika kuufunika msikiti huo lilitolewa wakati wa uchimbaji wa maandalizi ya ujenzi wake.

Msikiti huo una urefu wa mita 27 na mnara una ngazi ambazo humuwezesha kupanda juu kuadhini bila tatizo lolote.

3483774

Kishikizo: qatar mnara msikiti
captcha