IQNA

Jamii ya Waislamu

Usomaji Qur'ani wa kijana Mwafrika na mke wake mzungu aliyesilimu wavutia wengi + video

18:24 - August 15, 2023
Habari ID: 3477441
MITANDAONI (IQNA)- Klipu ya kijana Mwafrika akijaribu kumfundisha Qur'ani Tukufu  mke wake mzungu aliyesilimu imevutia hisia za watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Tovuti ya Dar al-Hilal imeripoti kuwa klipu hiyo iliyotumwa katika mitandao ya kijamii na kijana huyu, inamuonyesha akimfundisha mke wake aliyesilimu Qur'ani Tukufu.

Katika klipu hiyo, kijana huyu wa Kiafrika amesimama karibu na mkewe, ambaye inaonekana ni Mzungu akiwa  amevaa hijabu, ambapo anasoma Sura Nasr ya  na mkewe pia anajaribu kurudia licha ya ugumu wa kuitamka.

 

 

 

 

Kishikizo: silimu qurani tukufu
captcha