IQNA

Historia ya Uislamu

Usitishaji vita uliolenga kulinda maadili

21:24 - September 14, 2023
Habari ID: 3477597
TEHRAN (IQNA) – Moja ya matukio makuu katika maisha ya mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) Imam Hassan (AS) lilikuwa ni amani yake na Mu’awiya, mapatano ya amani ambayo yanaweza kuelezwa kuwa ni usitishaji vita uliokuwa na lengo la kulinda maadili na uwezo.

Kumekuwa na uchanganuzi usio wa haki uliofanywa katika historia kuhusu tukio hili.

Kwa sababu mbalimbali, Imam Hassan (AS) amedhulumiwa katika historia ya Uislamu. Baadhi ya sababu ni kama zifuatazo:

1- Siku yake ya kufa shahidi inasadifiana na kumbukumbu ya kufariki kwa Mtukufu Mtume (SAW) na ndiyo maana wahubiri wakati mwingi hawapati fursa kamili ya  kuzungumzia vya kutosha kuhusu maisha, tabia na fadhila za Imam Hassan (AS).

2- Riwaya zinasema kuwa mwili wa Imam Hassan (AS) ulipigwa na mishale zaidi ya 70. Mwili wake ulipopelekwa kwenye Haram Tukufu ya Mtume Muhammad (SAW) kuzikwa huko na wakati maandalizi yakiendelea, mwanamke mmoja aliyekuwa amepanda nyumbu alifika akidai kuwa hiyo ni nyumba yake na hakuna mtu atakayeruhusiwa kuuzika mwili wa marehemu Imam Hassan (AS) hapo.

3- Imamu Hassan (AS) hata alidhulumiwa nyumbani kwake kwani mke wake alimuua kwa amri ya Mu’awiya.

4- Suala kuu ambalo Imam Hassan (AS) amedhulumiwa nalo ni mapatano ya amani na Mu’awiya. Lau isingekuwa makubaliano hayo ya amani, Uislamu ungeangamizwa hapo hapo na hakuna kitu kingebakia katika historia.

5- Baadhi ya makamanda wa jeshi la Imam Hassan (AS) walimsaliti kwani walituma ujumbe wa maandishi kwa Mu’awiya, wakimtaka afanye mashambulizi na kuahidi kwamba watamsalimisha Imam Hassan (AS) kwa Mu’awiya au kumuua.

6- Wafuasi wake ambao wengi wao walikuwa watu wa Kufa waliasi dhidi yake na wakasema wanataka kuishi na hawataki kupigana, wakamshinikiza Imam Hassan (AS) kutia saini mkataba wa amani na Mu’awiya.

7- Waislamu wa madhehebu ya Shia wanajua zaidi kuhusu ukarimu wa Imam Ali na jinsi alivyosaidiwa na kuwasaidia mayatima na masikini, lakini wanajua kidogo juu ya juhudi za Imam Hassan (AS) za kuwasaidia masikini na kuwasaidia mayatima na vile vile juhudi zake za kuutetea Uislamu wa Kishia na kuwalinda Mashia.

3485155

Kishikizo: imam hassan as
captcha