Haya ni kwa mujibu wa mkurugenzi wa taasisi hiyo Hujjatul Islam Mojtaba Mohammadi alipokuwa akitangaza maelezo kamili ya mashindano hayo katika kikao na wanahabari siku ya Jumamosi.
Mashindano hayo yana kategoria mbili: Usomaji wa Qur'ani Tukufu kwa mbinu ya Taqlid kwa wanaume na kuhifadhi Qur'ani Tukufu kwa wanaume na wanawake.
Kategoria ya kisomo inawahitaji washiriki kuiga mojawapo ya visomo vinne vilivyochaguliwa vya maqari mashuhuri ambao ni Sheikh Mohamed Siddiq El-Minshawi, Sheikh Abdul Basit Abdul Samad, Sheikh Shahat Muhammad Anwar, na Sheikh Mustafa Ismail.
Ushindani uko wazi kwa waombaji kutoka kote ulimwenguni, lakini fainali ni mshiriki mmoja tu kutoka kila nchi atachaguliwa.
Hatua ya mwisho itafanyika katika Haram ya Imam Ridha AS huko Mashhad mnamo Januari 6-7.
Tarehe ya mwisho ya usajili ni Januari 20, na wagombea wanaotaka kushuriki wanaweza kutuma maombi kupitia tovuti hii ya Taasisi ya Qur'ani ya Meshkat.
Washindi wa kila kategoria watapata zawadi ya pesa taslimu karibu USD 2,000, huku watakaoshika nafasi za pili wakitazamiwa kupata karibu USD 1,600 na USD 1,400 mtawalia.
Toleo la awali la shindano hilo lililofanyika mwaka jana, lilivutia washiriki zaidi ya 1,000 kutoka nchi 73, kati yao 153 walifanikiwa kuingia hatua ya fainali.
4190864