IQNA

Watetezi wa Palestina

Maandamano ya Wananchi wa Bahrain ya kuunga mkono Palestina, Yemen

21:58 - January 20, 2024
Habari ID: 3478220
IQNA – Watu nchini Bahrain wameshiriki maandamano kueleza mshikamano wao na watu wa Palestina na wapiganaji wa Yemen.

Maandamano hayo yalifanyika al-Diraz, kaskazini magharibi mwa Bahrain, baada ya sala ya Ijumaa.

Waandamanaji hao wakiwa wamebeba bendera za Palestina walipiga nara za kuwaunga mkono wananchi wa Ukanda wa Gaza na kulaani vita vya mauaji ya kimbari vya utawala wa Kizayuni katika eneo hilo la pwani.

Aidha wameipongeza Yemen kwa kushambulia meli zinazomilikiwa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Bahari Nyekundu kuunga mkono watu wa Palestina.

Wananchi wa Bahrain walioshiriki katika maandamano hayo pia wameipongeza harakati ya muqawama ya Hizbullah ya Lebanon na Katibu Mkuu wake Sayed Hassan Nasrallah kwa kukabiliana na vitendo vya kichokozi vya utawala ghasibu wa Israel.

Mapema mwezi huu, Sayed Nasrallah amewapongeza wananchi wa Bahrain kwa kukataa misimamo ya utawala wa kifalme nchini humo dhidi ya Palestina na Yemen.

Tangu kuanza kwa vita vya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Gaza mwanzoni mwa mwezi Oktoba, na kama sehemu ya kuwaunga mkono Wapalestina, Vikosi vya Wanajeshi vya Yemen na Ansarullah katika Bahari Nyekundu au Bahari ya Sham vimelenga meli kadhaa za utawala katili wa Israel na zile zinazoelekea kwenye bandari za zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo.

3486875

Habari zinazohusiana
Kishikizo: bahrain palestina gaza
captcha