IQNA

Harakati za Qur'ani

Kitabu cha kuwasaidia wenye ulemavu wa macho kusoma nakala ya Qur'ani ya Braille

17:54 - April 02, 2024
Habari ID: 3478618
IQNA - Kitabu cha mwongozo cha kusoma nakala za nukta nundu (braille) za Qur'ani Tukufu kimezinduliwa nchini Indonesia.

Wizara ya Masuala ya Kidini ya nchi hii ya Kusini-Mashariki mwa Asia ilizindua kitabu cha mwongozo, kinachoitwa "Iqro'na,", kilichokusudiwa watu wenye ulemavu wa kuona ili iwe rahisi kwao kuelewa au kujifunza Qur'ani.

"Huu ni kielelezo cha kujifunza kwa wale wenye mahitaji maalum katika uwanja wa machi ili waweze kujifunza kwa urahisi nakala ya Qur'ani iliyoandikwa kwa Braille," Katibu Mkuu wa wizara hiyo M. Ali Ramdhani alisema huko Jakarta, Jumatatu, Aprili 01 , 2024.

Uzinduzi wa mwongozo huu wa usomaji wa Misahafu wa Braille umefanyika sanjari na Maonyesho ya Ramadhani yenye mada "Quran Kwa Wote" yaliyofanyika katika ofisi ya wizara huko Jakarta mnamo Aprili 1-3, 2024.

Ramdhani alisisitiza kuwa wizara hiyo ina nia ya dhati ya kuhakikisha kuwa Qur'ani inapatikana kwa pande zote, bila ubaguzi.

Kwa mujibu wa katibu huyo mkuu, wizara hiyo imewasilisha nakala ya Qur'ani ya Braille na kitabu chake cha mwongozo sio tu kwa Waislamu wa Indonesia bali pia kwa jamii ya Waislamu duniani kote.

"Kwa sababu lugha ya ishara na braille ni mbinu za kusoma zinazotumika kimataifa," alisema.

Mkuu wa Utafiti, Maendeleo, Elimu, na Mafunzo wa wizara hiyo, Amien Suyitno, alisema kuwa nakala ya Qur'ani ya Braille imechapishwa na kusambazwa kwa muda mrefu lakini si watu wengi wanaojua kuisoma.

Kwa hivyo, inatumainiwa kwamba uzinduzi wa kitabu cha mwongozo wa kusoma Msahafu wa  Braille utatoa ufikiaji mpana zaidi na kupunguza kiwango cha watu wasiojua kusoma nchini humo.

3487765

captcha