IQNA

Hafidh wa Misri, Qari wa Iran washinda mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya wanachuo

11:06 - January 05, 2015
Habari ID: 2672141
TEHRAN-IQNA- Mashindano ya 5 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo Waislamu yamemalizika Jumapili mjini Tehran huku wawakilishi wa Iran na misri wakichukua nafasi za kwanza katika qiraa na hifdhi kwa taratibu.../mh 2671946

Jopo la majaji lilitangaza kuwa Mohammad Abdul Aziz Niyazi kutoka Misri ndie mshindi katika kuhifadhi kikamilifu Qur'ani Tukufu. Mwakilishi wa Iran Mohammad Javad Mohammad Majd alichukua nafasi ya pili huku Mahmoud el-Kofri wa Lebanon akichukua nafasi ya tatu.
Katika kategoria ya Qiraa, Vahid Khazaei wa Iran akichukua nafasi ya kwanza huku maqarii kutoka Misri na Iraq wakichukua nafasi za pili na tatu kwa taratibu.
Duru ya Tano ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya wanachuo Waislamu imefanyika Tehran kwa kuhudhuriwa na washiriki 66 kutoka nchi 57 duniani.
Washiriki hao ambao ni  ni wanafunzi wa vyuo vikuu na walishindana kwa muda wa siku nne kusoma (qiraa) na kuhifadhi Qur'ani Tukufu katika mnara wa Milad mjini Tehran.../mh

2671946

captcha