IQNA

Taazia

Hafidh mkongwe zaidi wa Qur'ani huko Kafr El-Shaikh, Misri aaga dunia

18:21 - January 02, 2024
Habari ID: 3478132
IQNA - Mwanaume anayejulikana kama Hafidh mzee zaidi wa Qur'ani Tukufu katika Jimbo la Kafr El-Shaikh nchini Misri ameaga dunia katika mji aliozaliwa akiwa na umri wa miaka 90.

Sheikh Shawqi Abdul Ati Nasr alifariki kutokana na ugonjwa sugu, gazeti la Al-Yawm kila siku iliripoti.

Alitumia miongo minane ya maisha yake katika kuhudumia Qur'ani Tukufu na kutoa mafunzo kwa vizazi kadhaa vya wasomaji na wahifadhi Qur'ani.

Shawqi alizaliwa mwaka wa 1933 katika Kijiji cha Khatir katika Kaunti ya Billa ya Kafr El-Shaikh.

Alihifadhi Qur'ani Tukufu yote akiwa na umri wa miaka kumi na kisha akajiunga na Chuo cha Kiislamu cha Al-Azhar kama Hafidh wa Qur'ani Tukufu

Wahifadhi na wasomaji wengi wa Qur'ani kutoka Kafr El-Shaikh na sehemu nyinginezo za Misri walikuja kwake ili kuboresha ujuzi wao wa Qur'ani.

3486643

Kwa mujibu wa mtoto wake Issam, Shawqi alisoma Ayat al-Kursi muda mfupi kabla ya kifo chake.

Wasomaji na wahifadhi wengi wa Qur'ani Tukufu, akiwemo qari mashuhuri Sheikh Abul Ainain Shuaisha, wamelelewa katika Kaunti ya Billa ya Kafr El-Shaikh.

captcha