IQNA

Harakati za Qur'ani Misri

Misri yazindua Shirika Linalosimamia Shughuli za Wasomi wa Qur'ani

21:16 - February 20, 2023
Habari ID: 3476593
TEHRAN (IQNA)-Wizara ya Wakfu ya Misri imesema imeanzisha shirika la kusimamia wasomi maarufu wa Qur'ani na wale wenye vipaji vya Qur'ani katika nchi hiyo ya Kiarabu.

Wizara hiyo imesema katika taarifa yake kwamba chombo hicho kipya kinalenga kuimarisha uwezo wa vipaji vya Qur'ani Tukufu na kuvisaidia kiutamaduni, kifedha na kielimu.

Itasaidia pia katika kubainisha vipaji vya Qur'ani na wasomi katika nyanja kama vile kuhifadhi Qur'ani, mahubiri, Ibtihal na kuhubiri, taarifa hiyo iliongeza.

Wizara iliongeza kuwa kamati maalum pia imeundwa kuhusiana na suala hili, kulingana na Bawaba Al-Ahram Daily.

Maafisa wa Wizara ya Wakfu kama vile Hisham Abdul Aziz, mkuu wa idara ya masuala ya kidini, pamoja na shakhsia wa Qur'ani kama Sheikh Abdul Fattah al-Taruti na Khaled al-Jundi ni miongoni mwa wajumbe wa kamati hiyo, ilisema taarifa hiyo.

Iliendelea kusema kuwa shakhsia zaidi wa Qur'ani wa nchi hiyo wataongezwa kwenye kamati hiyo kadri itakavyohitajika.

Misri ni nchi ya Afrika Kaskazini yenye wakazi wapatao milioni 100. Waislamu ni takriban asilimia 90 ya watu wote wa nchi hiyo.

Shughuli za Qur'ani zimeenea sana katika nchi kaskazini mwa Afrika ambayo inawasomaji wengi zaidi wa Qur'ani ulimwenguni.

4123233

captcha