IQNA

Harakati za Qur'ani Misri

Misri kuzindua Msafara wa Qur'ani Mwezi wa Ramadhani

22:06 - March 03, 2024
Habari ID: 3478441
IQNA - Wizara ya Wakfu ya Misri inapanga kuzindua msafara wa wasomaji Qur'ani Tukufu kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani. Msafara huo utaundwa na Idara ya Wakfu ya Mkoa wa Alexandria.

Makari hao watatembelea misikiti tofauti katika eneo la mkoa katika usiku wa Ramadhani na kufanya duru za usomaji wa Quran.
Pia wataisoma Qur'ani Tukufu misikitini wakati wa swala ya Ijumaa katika mwezi mtukufu.
Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za wizara ya Awqaf zenye lengo la kuendeleza shughuli za  Qur'ani Tukufu katika mwezi wa mfungo.
Wakati huo huo, naibu Waziri wa Wakfu Sheikh Salamah alitembelea misikiti kadhaa wakati wa sala ya asubuhi ili kuhakikisha kuwa imesafishwa na iko tayari kuwakaribisha waumini katika Ramadhani. Misikiti yote nchini imeagizwa kufanya usafi mwezi mtukufu unapokaribia. Ramadhani (ambayo huenda ikaanza Machi 12 mwaka huu) ni mwezi wa tisa wa kalenda ya Kiislamu.
Ni kipindi cha sala, saumu, utoaji wa sadaka na uwajibikaji kwa Waislamu duniani kote.  

Mwezi wa Ramadhani, ambao mwaka huu huenda ukaanza Machi 11 mwaka huu kwa kutegemea mwezi mwandamo, ni mwezi wa tisa wa kalenda ya Kiislamu.

NI mwezi wa Saumu na kukithirisha ibada  pamoja na kutoa sadaka na uwajibikaji kwa Waislamu duniani kote.

Qur'ani Tukufu iliteremshwa kwenye moyo wa Mtukufu Mtume (SAW) katika mwezi huu.

Wakati wa Ramadhani, Waislamu hufunga (kujiepusha na vyakula na vinywaji) kuanzia Alfajiri hadi Magharibi.

Waislamu pia wanatumia muda mwingi katika mwezi huu kusoma Qur'ani Tukufu na kutafakari kuhusu aya zake.

Kishikizo: misri qurani tukufu
captcha