IQNA

Misri

Misri kuzindua mpango wa kuwafunza Maqari milioni watoto

17:32 - April 25, 2023
Habari ID: 3476913
TEHRAN (IQNA) - Wizara ya Wakfu ya ya Misri imesema mpango wa kutoa mafunzo kwa wahifadhi Qur'ani watoto milioni moja utazinduliwa nchini humo.

Wizara ilisema mpango huo utazinduliwa kwa mwaka wa pili mfululizo kukiwa na mabadiliko kadhaa, kulingana na Gazeti la Al-Ahram.

Mpango huo utaandaliwa kwa kushirikisha misikiti 20,000 kote nchini kwani pauni milioni 2 za Misri pia zimewekwa kama tuzo kwa washiriki.

Mpango huo unajumuisha mihadhara ya maadili pamoja na safari za kielimu kwa lengo la kubainisha vipaji katika nyanja ya usomaji wa Qur'ani, ibtihal na utamaduni wa kidini.

Wizara ilisema maelezo zaidi ya mpango huo yatatangazwa hivi karibuni.

Waziri wa Wakfu wa Misri, Mohamed Mokhtar Gomaa alisema mpango huo unalenga kuendeleza njia ya kukuza dini na kuitumikia Qur'ani iliyokuwa ikizingatiwa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Alibainisha kuwa mpango huo unalenga kuibua vipaji na kuwatayarisha kwa ajili ya kusimamia masuala ya misikiti huku pia wakiongeza idadi ya wasomaji qurani kote nchini.

3483324

captcha