IQNA

Watetezi wa Qur'ani

Washiriki mashindano ya Qur'ani Misri waandamana kutangaza mshikamano na Gaza

14:15 - February 03, 2024
Habari ID: 3478294
IQNA - Washiriki wa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani huko Port Said, Misri, walifanya maandamano ya kuwaunga mkono Wapalestina wanaodhulumiwa wa Gaza.

Awali walihudhuria sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Ash-Shati wa jiji hilo na kisha wakakusanyika kutoka msikitini hadi Uwanja wa Ash-Shuhada (Mashahidi) ili kupaza sauti ya mshikamano na watu wa Gaza, tovuti ya Cairo24 iliripoti.

Adil Muslihi, mkurugenzi mtendaji wa mashindano hayo, alisema mjumuiko huo unalenga kufikisha ujumbe kwa ulimwengu kwamba mauaji ya watu katika Ukanda wa Gaza lazima yakome na amani lazima itawale ulimwenguni.

Utawala wa Israel umewauwa zaidi ya watu 27,000 katika Ukanda wa Gaza tangu tarehe 7 Oktoba 2023. Mashambulio hayo ya kijeshi yamesababisha watu wengi kuyahama makazi yao na kuangamizwa na kuweka mazingira ya njaa huko Gaza.

Toleo la 7 la mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Port Said ilizinduliwa katika sherehe baadaye siku ya Ijumaa.

Waziri wa Wakfu wa Misri Sheikh Mohammed Mukhtar Gomaa na maafisa wengine kadhaa walihudhuria hafla ya ufunguzi.

Mashindano hayo yameandaliwa katika kategoria za kuhifadhi Qur'ani Tukufu na Ibtihal kwa msaada wa Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly.

Toleo la mwaka huu limepewa jina la qari maarufu wa Misri Sheikh Shahat Muhammad Anwar (1950-2008).

3487059

Habari zinazohusiana
captcha