IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Port Said Misri yamalizika

23:37 - February 07, 2024
Habari ID: 3478320
IQNA - Toleo la 7 la Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu na Ibtihal ya Port Said nchini Misri yalihitimishwa katika sherehe siku ya Jumanne. Washindi katika kategoria tofauti walitajwa na kutunukiwa katika hafla ya kufunga, tovuti ya Youm7 iliripoti.

Hafla hiyo ilianza kwa usomaji wa aya za Qur’ani Tukufu na hotuba ya gavana wa Port Said ambapo aliwashukuru waandaaji, jopo la majaji, washiriki na watazamaji.

Katika kipengele cha kuhifadhi Quran, Hareth Khaled Abdul Rahman kutoka Libya na Amina Khaled Abdul Aziz kutoka Misri kwa pamoja walishinda taji la kwanza na mshindi wa pili alikuwa Abdul Qadir Yusuf kutoka Somalia.

Katika kategoria qiraa, Isam Ahmed Hussein kutoka nchi mwenyeji, Ahmed Salim kutoka Tanzania na Tanwir Ahmed kutoka Bangladesh waliibuka wa kwanza hadi wa tatu mtawalia.

Katika Ibtihal, Muhammad Ridha Mahmoud wa Misri alinyakua tuzo ya juu na safu ya pili na ya tatu ilikwenda kwa Omar Abdul Nassir kutoka Lebanon na Ilyas Wardi kutoka Morocco.

Katika hafla hiyo wajumbe wa jopo la majaji akiwemo mwenyekiti Sheikh Abdul Karim Salih pamoja na Sheikh Abdul Fattah Taruti walitunukiwa pia.

Wanaharakati wa Qur'ani kutoka nchi 50 walishiriki katika toleo hili la tukio la kimataifa la Qur'ani.

Nchi zilizoshiriki ni pamoja na Tunisia, Algeria, Sudan, Falme za Kiarabu, Palestina, Jordan, Nigeria, Indonesia, Uganda, Pakistan, India, Marekani, Canada, Lebanon, Kenya, Yemen, na Ethiopia.

Toleo la mwaka huu lilipewa jina la qari maarufu wa Misri Sheikh Shahat Muhammad Anwar (1950-2008).

 

4198589

 

Habari zinazohusiana
captcha