IQNA

Hasira Zinazozidi Asia Magharibi huku Mashambulizi ya Israel Yakiua watu 500 katika Hospitali ya Gaza

15:01 - October 18, 2023
Habari ID: 3477756
TEHRAN (IQNA) - Waislamu katika nchi mbalimbali katika eneo la Asia Magharibi waliingia barabarani Jumanne usiku kukemea uhalifu wa hivi punde wa Israel katika kulenga hospitali ya kiraia katika Ukanda wa Gaza.

Shambulio baya la anga la Israel katika Hospitali ya Al-Ahli al-Arabi limeshangaza walimwengu na kuzidisha hasira dhidi ya utawala unaoukalia kwa mabavu wa Israel katika eneo la Asia Magharibi.

Tangu kuanza kwa mashambulizi ya anga ya Israel huko Gaza tarehe 7 Oktoba, makumi ya maelfu ya wakaazi wametafuta hifadhi katika hospitali ili kuepuka mashambulizi ya mabomu yanayoendelea, wakitafuta usaidizi na usalama.

Shambulio hilo liligharimu maisha ya Wapalestina wasiopungua 500 na lilishutumiwa vikali na mataifa katika eneo hilo.

Mashambulizi ya anga ya Israel katika hospitali ya Gaza yaua Wapalestina wasiopungua 500

Wakati huohuo, watu nchini Iran, Jordan, Uturuki, Lebanon na Iraq, na vilevile katika Ukingo wa Magharibi, walikusanyika mitaani saa chache baada ya shambulio hilo baya kuelezea hasira zao.

Maandamano yamezuka katika takriban nusu ya miji nchini Iran kufuatia shambulio la hospitali, Katika mji mkuu wa Tehran, waandamanaji waliandamana kutoka Medani ya Palestina hadi Ubalozi wa Ufaransa, wakiimba nara za kupinga uvamizi huo na uungaji mkono wa Magharibi kwa hilo.

Maandamano pia yanapangwa kufanyika mjini Tehran siku ya Jumatano kulaani tukio hilo.

Huko Istanbul, mvutano ulionekana wakati waandamanaji walipojaribu kuingia kwenye ubalozi mdogo wa Israel, na kusababisha polisi wa Uturuki kuwatawanya watu na kulinda eneo hilo.

Huko Amman, Jordan, waandamanaji wengi walifanya jaribio la kuvunja ubalozi wa Israel lakini wakasukumwa na polisi ambao walitumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya umati huo wenye hasira.

Mauaji ya Wazayuni ya Wagonjwa, Wafanyikazi wa Matibabu katika Hospitali ya Gaza Yaleta Laana ya Ulimwenguni

Siku ya Jumanne, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei alisisitiza jinai zinazoendelea za Israel zimezifanya mataifa ya Kiislamu kuwa na hasira na kuongeza, Iwapo jinai hizi zitaendelea, Waislamu na vikosi vya upinzani vitakosa subira, na hakuna atakayeweza kuwazuia.

 

3485636

captcha