IQNA

Jinai za Israel

Hamas yalaani mpango wa Israel wa kuwafurusha wakazi wa Gaza, yasema ni jinai ya kivita

15:44 - January 01, 2024
Habari ID: 3478128
IQNA-Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, imeashiria mpango wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa kuwafukuza kwa umati Wapalestina katika Ukanda wa Gaza na kutahadharisha kuwa, pendekezo la viongozi wa utawala huo wa Kizayuni la kutaka kupunguzwa idadi ya wakazi wa Gaza ni jinai ya kivita.

Hamas imesema katika taarifa kuwa, pendekezo la Waziri wa Fedha wa Israel, Bezalel Smotrich la kutaka eti kupunguzwa idadi ya wakazi wa Gaza kwa milioni 2 na kubakisha laki 2 pekee linakusudia kuandaa mazingira ya kurejea walowezi wa Kizayuni wenye misimamo mikali katika eneo hilo baada ya vita.

Jana Jumapili, Smotrich ambaye pia ni kiongozi wa chama cha misimamo mikali ya mrengo wa kulia  ya Uzayuni wa Kidini alisema kuwa, Wapalestina wa Gaza wamekuwa wakiishi kwenye mabanda kwa zaidi ya miaka 75, na wenyewe wanataka kuondoka, na eti wanapasa kushajiishwa kuhama.

Hamas imejibu bwabwaja hizo kwa kusema, "Watu wetu wameshachukua msimamo. Watasimama kidete mkabala wa juhudi zozote za kuwafurusha kutoka kwenye ardhi na nyumba zao, mpaka pale ukombozi kamili wa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu utakapotimia, na kurejea kwa wakimbizi wote.

Wakati huo huo, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Mahmoud Abbas amesema Wapalestina wataendelea kusimama kidete na kulinda haki zao za halali, na kamwe hawataruhusiwa kufukuzwa kwenye ardhi za mababu zao.

Kwa mujibu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina la Umoja wa Mataifa UNRWA, vita vya Israel vimefanya watu karibu milioni 2 kuhama makazi yao huko Gaza tangu Oktoba 7 mpaka sasa. 

Haya yanaripoti wakati huu ambapo tayari asilimia 70 ya nyumba na majengo katika Ukanda wa Gaza zimebomolewa kufuatia mashambulizi ya pande zote ya utawala wa Kizayuni katika eneo hilo.

3486640

Habari zinazohusiana
captcha