IQNA

Jinai za Israel

Umoja wa Mataifa: Israel inazuia misaada Gaza huku ikiendeleza mauaji ya kimbari

17:58 - January 16, 2024
Habari ID: 3478204
IQNA - Shirika la Umoja wa Mataifa la kutoa misaada ya kibinadamu (OCHA) liliripoti kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel umeendelea kuzuia utoaji wa misaada muhimu ya kibinaadamu ikiwa ni pamoja na dawa muhimu na mafuta ya kuendesha huduma za maji na usafi wa mazingira kaskazini mwa Gaza.

Shirika hilo lilionya kwamba ukosefu wa vifaa hivi unaleta hatari kubwa za kiafya kwa watu waliozingirwa.

Kwingineko, Philippe Lazzarini, Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA), amesema siku 100 zilizopita za mashambulizi ya Israel huko Ukanda wa Gaza zimekuwa kama miaka 100 kwa watu wa Gaza.

Lazzarini amesema hayo kwa mnasaba wa kupita siku 100 tangu Israel ianze kuwashambulia wakazi wa Ukanda wa Gaza kwa mabomu, mizinga na ndege za kivita akisisitiza kwamba, Wapalestina wamelazimika kuyahama makazi yao kwa wingi zaidi tangu mwaka 1948 kutokana na mashambulizi hayo. Lazzarini ameongeza kuwa "watu milioni 1.4 wamekimbilia kwenye vituo vya UNRWA na wanalazimishwa kuishi katika mazingira yasiyo ya binadamu."

Aisa huyo wa Umoja wa Mataifa amesema: "Katika muda wa siku 100 zilizopita, Gaza imeshuhudia “sura mbaya ya mauti, uharibifu, kulazimishwa watu kuwa wakimbizi, njaa, hasara na mateso ambavyo vinatia doa ubinadamu wetu.”

Amesema kwamba "siku 100 zilizopita ni kama miaka 100 kwa wakazi wa Gaza," na kuongeza kwamba, watu wengi wa Gaza watakuwa na majeraha ya kimwili na kisaikolojia ya kudumu katika maisha yao yote kutokana na mashambulizi ya Israel.

Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa, idadi ya Wapalestina waliouawa shahidi katika mashambulio ya kinyama ya mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza tangu tarehe 7 Oktoba hadi sasa imekaribia 24,000 na idadi ya majeruhi ni 60,500.

3486832

Habari zinazohusiana
captcha