IQNA

Jinai za Israel

'Ni magaidi pekee wanaofanya hivi': Hamas yalaani wanajeshi wa Israel wanaowadhalilisha raia Gaza

20:05 - December 08, 2023
Habari ID: 3478007
GAZA (IQNA)-Harakati ya Kiisalmu ya Kupigania Ukombozi wa Palestina, Hamas, imelaani vikali vikosi vya utawala haramu kwa kuwakamata na kuwanyang'anya mali raia waliokimbia makazi yao katika shule moja katika Ukanda wa Gaza.

Hamas ilisema katika taarifa yake kwamba vitendo vya jeshi la Israel ni "uhalifu wa wazi wa Wazayuni" na "kitendo ambacho kinaweza tu kufanywa na mamluki na magaidi  wasio na maadili yoyote."

Hamas imetaka "mashirika yote ya haki za binadamu na taasisi za kibinadamu kuingilia kati" na kusimamisha unyanyasaji wa utawala wa Israel dhidi ya raia wa Palestina.

Watumiaji wa mitandao ya kijamii walisambaza picha za makumi ya wanaume wa Kipalestina wakiwa wamevalia nguo zao za ndani  tu wakiwa wanashikiliwa mateka na wanajeshi katili wa Israel siku ya Alhamisi.

Miongoni mwa waliokamatwa na kupekuliwa ni Diaa al-Kahlout, mwandishi wa habari wa Palestina anayefanya kazi na Alaraby Aljadeed.

Hamas pia imewaomba wapigania uhuru na wanaharakati na wapigania ukombozi kote duniani kuendeleza shughuli zao za kiraia za kulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel na kuonyesha mshikamano na wananchi wa Palestina, lengo likiwa ni kukomesha mashambulizi ya utawala wa Kizayuni na mauaji ya kizazi dhidi ya raia wa Palestina wakiwemo watoto na wanawake.  

Utawala ghasibu wa Israeli umekuwa ukishambulia kwa mabomu na makombora Ukanda wa Gaza tangu Oct. 7, na kuua Wapalestina wasiopungua 17,500 na kujeruhi wengine zaidi ya 46,000, kulingana na vyanzo vya Palestina.

3486333

Habari zinazohusiana
Kishikizo: jinai za israel gaza
captcha