IQNA

Jinai za Israel

Israel inawaua kwa makusudi maprofesa Wapalestina ili kuangamiza Gaza kielimu

13:25 - January 22, 2024
Habari ID: 3478233
IQNA-Utawala wa Kizayuni wa Israel umewauwa maprofesa 94 wa vyuo vikuu, mamia ya walimu, na maelfu ya wanafunzi katika Ukanda wa Gaza katika muda wa miezi mitatu, kwa mujibu wa shirika moja huru la kutetea haki za binadamu.

Shirika hilo lijulikanalo kama, Euro-Med Human Rights Monitor, katika taarifa yake mpya limebaini kwamba, jeshi katili la Israeli lililenga wasomi, wanasayansi na wataalamu katika ukanda huo katika "mashambulio ya makusudi na mahususi ya anga kwenye nyumba zao bila taarifa ya hapo awali."

"Takwimu zinaonyesha kuwa hakuna uhalali au sababu ya wazi ya kulenga watu hawa," iliongeza taarifa ya shirika hilo lenye makao yake Geneva.

Takriban Wapalestina 25,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, hadi sasa wameuawa na utawala dhalimu wa Israel tangua uanzishe vita vya maangamizi ya umati dhidi ya Ukanda wa Gaza Oktoba saba mwaka jana.

Kulingana na Euro-Med, utawala vamizi wa Israel umeharibu kila chuo kikuu katika Ukanda wa Gaza wakati wa kampeni ya vita vya maangamizi ya umati dhidi ya eneo hilo la Palestina.

Kwingineko katika taarifa yake shirika hilo limeinukulu Wizara ya Elimu ya Palestina yenye makao yake makuu Gaza ikitangaza kuwa mashambulizi hayo yamepeleka  kuuawa walimu na wasimamizi 231 pamoja na wanafunzi wasiopungua 4,327.

"Uharibifu mkubwa na wa kimakusudi wa Israeli wa mali za kitamaduni na kihistoria za Wapalestina, ikiwa ni pamoja na vyuo vikuu, shule, maktaba, na hifadhi za kumbukumbu, unaonyesha sera yake ya kulifanya eneo la Gaza kuwa lisiloweza kukalika," Euro-Med imeonya.

Said Arikat, mwandishi wa habari na profesa msaidizi katika Chuo Kikuu cha Marekani huko Washington D.C., alisema uharibifu uliofanya na utawala haramu wa Israeli  dhidi ya sekta ya elimu ya juu huko Gaza ulikuwa "wa kiitikadi" na "makusudi".

Akizungumza na Al Jazeera kutoka Washington D.C., Bw. Arikat alisema "ni dhahiri kwamba Israel inafanya mauaji ya kitamaduni huko Gaza".

Katika moja ya shambulio la hivi punde dhidi ya vituo vya elimu, vikosi vya Israel vilivyokaliwa kwa mabavu siku ya Jumatano viliripua Chuo Kikuu cha Al-Israa huko Gaza baada ya kukikalia kwa siku 70. Chuo kikuu kilitoa kozi ikijumuisha sheria ya uhandisi wa fedha kwa wanafunzi zaidi ya 4,000.

/3486888

Habari zinazohusiana
captcha