IQNA

Jinai za Israel

Mpalestina aliyepigwa risasi na askari katili wa Israel alifariki kutokana na majeraha

8:08 - August 19, 2023
Habari ID: 3477459
Al- AQSA (IQNA)- Kijana wa Kipalestina ameaga dunia kutokana na majeraha ya risasi aliyopigwa na wanajeshi wa utawala haramu Israel miaka miwili iliyopita wakati wa uvamizi wa kikatili wa Israel kwenye Msikiti wa al-Aqsa mjini Quds (Jerusalem).

Kwa mujibu wa taarifa Hamza Abu Sneineh aliyekuwa na umri wa miaka 30 siku ya Ijumaa asubuhi. Sneineh alipata majeraha mabaya pale risasi ilipomtoboa fuvu la kichwa wakati wa uvamizi mkali wa Mei 7, 2021, ulioambatana na Laylat al-Qadr, siku muhimu kwa Waislamu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Katika uvamizi huo, wanajeshi katili wa Israel walitumia gesi ya kutoa machozi, risasi za chuma zilizoezekwa na mpira dhidi ya waumini, na hivyo  kusababisha mamia ya Wapalestina kujeruhiwa.

Sneineh alipasuka i fuvu la kichwa na kupoteza jicho lake la kushoto kutokana na uvamizi huo. Alikimbizwa katika katika Hospitali ya Hadassah Ein Kerem huko al-Quds kwa matibabu. Licha ya hali yake mbaya, vikosi vya Israel vilimkamata siku kadhaa baadaye, na kumwachilia baadaye.

Vyanzo vya kimatibabu vimeripoti kuwa Sneineh alikuwa akipata maumivu makubwa kutokana majeraha yake kwa muda wa miezi huku afya yake ikizorota kwa kiasi kikubwa wiki kadhaa kabla ya kifo chake.

Vitendo vya mara kwa mara vya ukatili dhidi ya waumini wa Kipalestina katika Msikiti wa al-Aqsa mwezi Mei 2021 vilisababisha vita vya siku 11 kati ya makundi ya kupigania ukombozi wa Palestina katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa na utawala haramu wa Israel. Wakati wa mzozo huu, vikosi vya Israeli viliwaua shahidi Wapalestina wasiopungua 260, wakiwemo watoto 66.

Maafisa wa Israel wenye misimamo mikali na walowezi mara kwa mara huvamia Msikiti wa Al Aqsa, kitendo cha uchochezi kinachowakasirisha Wapalestina. Uvamizi huu mara nyingi hupangwa na magenge ya  walowezi wa Kizayuni wanaoungwa mkono na utawala haramu wa Israel.

Kwa mujibu wa makubaliano kati ya Jordan, mlinzi wa maeneo ya Kiislamu na Kikristo huko al-Quds, na Israel kufuatia kukalia kwa mabavu al-Quds Mashariki mwaka 1967, ibada zisizo za Kiislamu katika msikiti huoo ni marufuku. Pamoja na hayo  makundi yenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia yametoa ya Kizayuni yana mpango hatari wa kugeuza al-Aqsa kuwa eneo la ibada ya Kiyahudi na kubomoa msikiti huo mtakatifu katika Kiislamu ili kujenga hekalu la Kiyahudi kwenye eneo hilo.

3484823

Habari zinazohusiana
Kishikizo: jinai za israel
captcha