IQNA

Harakati za Qur'ani Tukufu

Mamia ya Wahifadhi wa Qur'ani Tukufu waenziwa katika Jimbo la Faiyum nchini Misri

10:40 - September 17, 2023
Habari ID: 3477613
CAIRO (IQNA) - Hafla imefanyika katika mji wa Itsa, Jimbo la Faiyum nchini Misri, kuwaenzi wahifadhi 989 wa Qur'ani Tukufu.

Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar kiliandaa hafla hiyo kwa ushirikiano na Shule ya Ahl al-Quran, yenye uhusiano na idara ya Wakfu ya mkoa.

Miongoni mwa waliotunukiwa kwa ufaulu wao ni wavulana na wasichana 350 ambao wameweza kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu 

Wengine wote wameweza kuhifadhi nusu au robo ya Qur'ani Tukufu.

Idadi ya wasomi na wanafikra wa Misri, maafisa wa Al-Azhar, wawakilishi wa vyombo vya habari na makundi mengine ya watu walihudhuria sherehe hiyo.

Misri ni nchi ya Afrika Kaskazini yenye wakazi wapatao milioni 100. Waislamu ni takriban asilimia 90 ya watu wote wa nchi hiyo.

Shughuli za Qur'ani Tukufu zimeenea sana katika nchi hii ambayo ina miongoni mwa wasomaji bora zaidi wa Qur'ani Tukufu.

Hundreds of Quran Memorizers Honored in Egypt’s Faiyum Governorate

4169180

Habari zinazohusiana
Kishikizo: misri qurani tukufu
captcha