IQNA

Chama tawala Afrika Kusini, ANC, kuendelea kuunga mkono Wapalestina

9:03 - February 08, 2015
Habari ID: 2822420
Chama tawala cha ANC nchini Afrika Kusini kimetangaza kuendeleza sera ya kuunga mkono mapambano ya Wapalestina ambao wanapigania kuikomboa ardhi yao inayokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.

Katika taarifa, mwanachama mwandamizi wa ANC ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani Afrika Kusini Malusi Gigaba amesema watu wa Afrika Kusini hasa wafuasi wa ANC wataendelea kuunga mkono harakati za ukombozi wa Palestina hata kama itachukua muda mrefu. Ameyasema hayo mjini Pretoria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo wakati akimkaribisha mwanaharakati mkongwe wa Palestina Leila Khaled. Amesema Afrika Kusini inasimama bega kwa bega na Wapalestina ambao wanadhulimuwa wakati wanapotafuta haki na uadulifu. Amesema mapambano ya Wapalestina ni sawa ya wazalendo wa Afrika Kusini ambao pia walipambana kwa muda mrefu dhidi ya utawala wa makaburu wabaguzi wa rangi. Gibaga ameongeza kuwa Afrika Kusini  itaendelea kuwaunga mkono Wapalestina kikamilifu na kuongeza kuwa  chama  cha ANC hakitabadilisha msimamo wake imara wa kutetea haki za taifa la Palestina.  Chama cha ANC kinaunga mkono kampeni za kususiwa utawala wa Kizayuni wa Israel.  Naibu Mwenyekiti wa zamani wa chama hicho, Baleka Mbete amenukuliwa akisema utawala wa Israel ni  mbaya zaidi kuliko hata utawala wa ubaguzi wa rangi wa makuburu uliokuweko huko Afrika Kusini.../mh

2819054

 

captcha