IQNA

Iran itakuwa kitovu cha utalii halali

16:39 - February 28, 2015
Habari ID: 2910925
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inatekeleza mkakati wa kuhakikisha inageuka na kuwa kitovu cha utalii halali kwa lengo la kuwavutia Waislamu milioni 15 kutoka maeneo mbali mbali duniani.

Hayo yamedokezwa na Makamu wa Rais wa Iran ambaye pia ni Mkuu wa Shirika la Turathi za Utamaduni Massoud Soltanifar ambaye amesema Iran itashuhudia ongezeko la watalii katika mustakabali.
Amesema mwaka jana watalii milioni tano wa kigeni waliitembelea Iran mwaka jana huku nusu yao wakielekea katika miji ya Mashhad na Qom kwa lengo la kuzuru maeneo matakatiu ya Waislamu wa madhehebu ya Shia.
Soltanifar amesema  serikali yake ina mpango maalumu wa kupanua  utalii halali. 'Hatua imara zikichukuliwa, Iran itawavutia watalii wa kigeni wapatao milioni 10-15 kwa mwaka.
Utalii halali unawalenga Waislamu na familia zao kutokana na kuwa katika utalii huu hoteli haziuzi pombe na kuna sehemu maalumu za wanawake na wanaume katika maeneo mbali mbali ya starehe kama vile kuogelea. Soltanifar amesema Iran inalenga kuwavutia watalii wa kigeni milioni 20 katika kipindi cha miaka 11 ijayo. Watalii hawa wanatazamiwa kutoka maeneo yote ya dunia hasa Asia, Afrika, Mashariki ya Kati na Ulaya. Mbali na maeneo ya kidini, Iran pia ina vivutio vingi vya utalii ikiwa ni pamoja na pwani ya Ghuba ya Uajemi kusini mwa nchi na Bahari ya Kaspi kaskazini mwa nchi. Aidha nchi hii ina milima na maeneo maalumu ya michezo ya misimu wa baridi na joto. Aidha kutokana na ustaarabu wake wa kale, Iran ina maeneo mengi ya historia ya kabla na baada ya Uislamu na watalii wanaweza kuona vivutio vingi hasa vya usanifu majengo.../mh
2890395

captcha