IQNA

‘Maisha ya Waislamu ni Muhimu Pia’

9:23 - August 17, 2016
Habari ID: 3470526
Mshukiwa mmoja amefikishwa mahakamani Marekani baada ya kubainika kuwa alimpiga risasi na kumua Imamu wa msikiti na Mwislamu aliyekuwa naye huko mjini New York huku Waislamu wakitaka uadilifu na haki.

Oscar Morel Mmarekani mwenye asili ya Kihispania mwenye umri wa miaka 35 kutoka Brooklyn alifikishwa mahakamani kwa mashtaka mawili ya mauaji na kumiliki silaha kinyume cha sharia.

Ikumbukwe kuwa Imam Alala Uddin Akongi wa Msikiti wa Jamia wa Al-Furqan na msaidizi wake aliyetambulika kama Thara Uddin waliuawa kwa kufyatuliwa risasi Jumamosi walipokuwa wakitoka kuswali swala ya Adhuhuri katika barabara ya Ozone, mji wa Borough of Queens jimboni New York.

Baraza la Mahusiano ya Kiislamu na Marekani limelaani mauaji hayo na kusema kuwa wawili hao mbali na kuwa viongozi wa kidini, walikuwa viongozi wa kijamii katika mji huo.

Waislamu wa eneo hilo walikutana Jumatatu katika eneo uwanja wa kuegeshea magari wa Queens na kuwasalia sala ya Janaza waliouawa.

Washiriki walisema Maisha ya Waislamu ni Muhimu huki wakitaka uadilifu ufanyike.

katika miezi ya hivi karibuni vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu vimeongezeka mno nchini Marekani na barani Ulaya.

Pamoja na kuwepo propaganda chafu dhidi ya Uislamu lakini idadi ya watu wanaosilimu na kuingia katika dini hii tukufu imekuwa ikiongezeka kwa kasi mno katika ulimwengu wa Magharibi.

3460715

captcha