IQNA

Mashindano ya Uchoraji kwa Kuzingatia Qur'ani yafanyika Afrika Kusini+PICHA

18:35 - November 23, 2016
Habari ID: 3470692
IQNA-Mashindano ya uchoraji kwa kuzingatia ufahamu wa Aya za Qur'ani kwa mtazamo wa watoto Waislamu yamefanyika Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa mwadishi wa IQNA, mashindano hayo yamefanyika kwa himaya ya Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Afrika Kusini kwa munasaba wa Siku ya Kimataifa ya Watoto ambayo huadhumishwa Novemba 20.

Watoto Waislamu walioshiriki katika mashindano hayo wamechora michoro mbali mbali kwa mujibu wa ufahamu wao kuhusu maudhui kadhaa za aya za Qur'ani . Mashindano hayo yalifanyika kwa ushirikiano baina ya Mwambata wa Utamaduni wa Iran na Shule ya Winterveld mjini Pretoria.

Akifafanua zaidi kuhusu Mashindano hayo yaliyowashirikisha watoto Waislamu zaidi ya 100 , Mwambata wa Utamaduni wa Iran mjini Pretoria Bw. Shahrouz Falahatpisheh alisema kuwa, "ufahamu sahihi kuhusu aya za Qur'ani na kuleta uhusiano baina ya maisha ya kawaida na aya hizo tukufu ni jambo lenye umuhimu mkubwa katika malezi ya watoto."

Ameongeza kuwa masuala kama vile ustawi endelevu, mazingira, umuhimu wa maji n.k ni masuala yanyojadiliwa sasa duniani na aya kadhaa za Qur'ani zimeashiria masuala hayo. Falahatpisheh amesema watoto hao wamejifunza kuhusu ufahamu na madhumuni ya aya zifuatazo: Aya ya 31 ya Surat Al-A'raaf, Aya ya 30 ya Suratul Anbiyaa Aya ya 30 na Aya ya 13 Surat Al H'ujuraat. Amesema aya hizo zinaashiria kuhusu maendeleo endelevu, umuhimu wa maji duniani na kuwepo anuai ya viumbe.

Watoto 10 bora katika mashindano hayo walitunukiwa zawadi kutoka Mwambata wa Utamaduni wa Iran.

Mashindano ya Uchoraji kwa Kuzingatia Qur'ani yafanyika Afrika Kusini+PICHA

3548005

captcha