IQNA

Turathi ya Uislamu

Nakala kongwe zaidi ya Qur'ani Tukufu Afrika Kusini: Jinsi Waislamu Wanavyoihifadhi

16:03 - August 25, 2023
Habari ID: 3477493
CAPE TOWN (IQNA) – Msahafu (Nakala ya Qur'ani Tukufu) kongwe zaidi nchini Afrika Kusini, ambayo imehifadhiwa katika eneo salama katika Msikiti wa Auwal wa Cape Town, ni hazina ya thamani kwa Waislamu wanaoithamini kama sehemu ya urithi wao tajiri.

Msahafu huo uligunduliwa katikati ya miaka ya 1980 kwenye dari ya Msikiti wa Auwal wakati wa juhudi za ukarabati.

Ukiwa na maandishi mazuri zaidi ya miaka 200 iliyopita, watafiti wanaamini kwamba Imam Abdullah ibn Qadi Abdus Salaam, anayejulikana kama Tuan Guru au Mwalimu Mkuu, aliandika Msahafu huo yeye binafsi bila kusoma mahala popote kwani alikuwa Hafidh wa Qur'ani Tukufu. Imedokezwa kwamba alifanya kazi hiyo baada kufukuzwa kutoka Indonesia  hadi Afrika Kusini na wakoloni wa Uholanzi.

Wajenzi waliipata kwenye mfuko wa karatasi katika dari ya Msikiti wa Auwal, walipokuwa wakiivunja kama sehemu ya ukarabati katikati ya miaka ya 1980.

"Kulikuwa na vumbi sana, ilionekana kana kwamba hakuna mtu aliyefikakwenye dari hiyo kwa zaidi ya miaka 100," Cassiem Abdullah, mjumbe wa kamati ya msikiti.

"Wajenzi pia walipata sanduku la maandishi ya kidini yaliyoandikwa na Tuan Guru." Nakala, iliyoandikwa kwa wino mweusi na mwekundu na ilikuwa katika hali nzuri ya kushangaza.

Juhudi za kuiunganisha ilikuwa ni matokeo ya kazi ya miaka mitatu iliyoongozwa na Maulana Taha Karaan, mwanasheria mkuu wa Baraza la Mahakama ya Waislamu lenye makao yake mjini Cape Town, kwa ushirikiano na wanazuoni kadhaa wa ndani wa Qur'ani Tukufu.

Mwandishi wa wasifu wa Tuan Guru, Shafiq Morton, anaamini kwamba Tuan Guru alianza kuandika nakala ya kwanza kati ya tano alipokuwa akizuiliwa kwenye Kisiwa cha Robben.

Kuinua roho ya watumwa

“Naamini moja ya sababu alizoandika Qur’an ilikuwa ni kuinua roho za watumwa waliomzunguka. Alitambua kwamba kama angeandika nakala ya Qur’an angeweza kuwaelimisha watu wake kutoka kwayo na kuwafundisha utu kwa wakati mmoja,” Morton anasema.

"Ukienda kwenye hifadhi na kuangalia karatasi ambayo Waholanzi walitumia, inafanana sana na ile iliyotumiwa na Tuan Guru. Pengine ni karatasi sawa.

"Kalamu zake angetengeneza mwenyewe kwa mianzi, na wino mweusi na mwekundu ungekuwa rahisi kupata kutoka kwa mamlaka ya kikoloni."

Changamoto kubwa kwa jamii ya Waislamu wa eneo hilo katika azma yao ya kuhifadhi moja ya vitu vya sanaa vya thamani kubwa katika urithi wao wa kale, ambao ulianza mwaka 1694, ilikuwa ni kuhakikisha kwamba kurasa zote zenye Aya zaidi ya 6,000 za Quran zinawekwa katika mpangilio sahihi.

Jukumu hili lilifanywa na marehemu Maulana Taha Karaan, ambaye alikuwa mwanasheria mkuu wa Baraza la Mahakama ya Waislamu lenye makao yake mjini Cape Town, kwa kushirikiana na wasomi kadhaa mahiri wa Qur'ani. Mchakato mzima, ambao ulihitimishwa kwa kufunga kurasa, ulichukua miaka mitatu kukamilika.

Tangu wakati huo Quran imeonyeshwa katika Msikiti wa Auwal, ambao ulianzishwa na Tuan Guru mnamo 1794 kama msikiti wa kwanza katika ambayo sasa ni Afrika Kusini.

Shaykh Owaisi, mhadhiri wa historia ya Kiislamu ya Afrika Kusini ambaye amefanya utafiti wa kina kuhusu Qur’ani zilizoandikwa kwa mkono mjini Cape Town, ameongeza kuwa, Tuan Guru aliandika nakala hizo ili kuhifadhi Uislamu miongoni mwa wafungwa na watumwa Waislamu.

'Hadithi ya ujasiri'

“Walipokuwa wakihubiri Biblia na kujaribu kuwabadili watumwa Waislamu, Tuan Guru alikuwa akiandika nakala za Qur'ani, akiwafundisha watoto na kuwafanya wazihifadhi aya.

"Inasimulia hadithi ya ujasiri na uvumilivu. Inaonyesha kiwango cha elimu cha watu walioletwa Cape Town kama watumwa na wafungwa.”

Jambo la kushangaza ni kwamba, kufukuzwa kwa Tuan Guru kusini mwa Afrika kulisababisha kuenea kwa Uislamu katika sehemu hii ya dunia, ambapo Waislamu sasa wanaunda karibu 5% ya watu wanaokadiriwa kuwa milioni 4.6 wa Cape Town.

"Alipokuja Cape, Tuan Guru aliona kuwa Uislamu ulikuwa katika hali mbaya sana hivyo alikuwa na kazi nyingi ya kufanya," Morton anasema. "Jumuiya haikuwa na mikono yao kwenye maandishi yoyote - walikuwa Waislamu zaidi kutoka kwa kumbukumbu za kitamaduni kuliko kitu kingine chochote.

"Ningesema kwamba hiyo Qur'an ya kwanza aliyoiandika ndiyo sababu kwa nini jamii ya Kiislamu ilisalimike na kuwa jamii inayoheshimika tuliyo nayo leo."

/3484917

captcha